- Mifugo

Mazao ya kilimo hai yanahitaji virutubisho vya asili

Sambaza chapisho hili

Kabla ya yote, ni muhimu mkulima kujiuliza na kufahamu ni namna gani virutubisho vya asili vya mimea hufanya kazi?

Mimea ya kijani ina uwezo wa kufanya (photosynthesis). Mwanga wa jua, hewa ya ukaa pamoja na maji huzalisha chakula cha mimea aina ya wanga, ambacho baadaye husafirishwa sehemu mbalimbali za mimea na kuhifadhiwa kwa namna ya wanga (carbohydrates).

Chakula hicho hutumiwa na mimea. Pia mimea ina uwezo wa kutumia wanga na madini/virutubisho vya aina mbalimbali mfano nitrojeni,salfa na madini joto kutengeneza vyakula aina mbalimbali mfano protini, mafuta na vitamin.

Tunaweza kusema mimea ni viwanda vya asili vinavyotengeneza vyakula vinavyoliwa na mimea yenyewe pamoja na wanyama na binadamu.

Binadamu na wanyama hutegemea kupata virutubisho kwa kula na kumeng’enya mimea au wanyama wengine wanaokula mimea tu (herbivorus).

Binadamu na wanyama hupata madini kutokana na vyakula wanavyokula. Mimea inapata madini na virutubisho vingine kutoka kwenye udongo, hewa na maji.

Hii hutegemea mzunguko mzima wa ikolojia, ambayo viumbe wadogo waliomo ardhini wanakuwa wanajishughulisha kujilisha kwa kutumia viini asili na visivyo vya asili kutoka ardhini na kuvigeuza kuwa katika hali ya kemikali.

Utunzaji wa virutubisho vya asili: “Lisha udongo na si mimea”

Elimu hii ya virutubisho asilia kwa mimea ni kutunza viumbe hai waliomo ardhini kwa sababu ni muhimu na wana jukumu la kutengeneza virutubisho ambavyo mimea hutegemea.

Mkulima anayefanya kilimo hai anaamini kuwa hii inawezekana tu kwa kurutubisha na kuutunza udongo vizuri kwa kutumia mbolea zenye virutubisho vya asili.

Wakulima wanaozalisha kwa kutumia misingi ya kilimo hai ni lazima waimarishe na kuboresha udongo na ni lazima kusheheneza walichovuna.

Kushindwa kutunza udongo na mazingira kwa ujumla inavyotakiwa haikubaliki katika kilimo hai na akitakuwa endelevu (sustainable) na udongo huchakaa haraka.

Rutuba kwenye udongo inaweza kutengenezwa kwa kutumia mzunguko wa masalia ya mimea na wanyama, ambao huongeza woevu kwenye udongo.

Masalia ya asili ni nguzo muhimu ya rutuba kwenye udongo. Virutubisho vinavyotokana na viumbe hai ni muhimu sana kwa udongo uliochakaa. Mbolea za chumvi chumvi zilizo nyingi zina athari mbalimbali katika udongo ingawa hutoa mavuno mengi.

Mbole za asili

Kwenye kilimo hai, mbolea ni lazima ziwe za asili. Mbolea hizo ni lazima ziwe zinatokana na mimea na wanyama (mbolea za mifugo, mbolea vunde, na mboji) ambazo zinakuwa na uwiano wa virutubisho tofauti na ilivyo kwa mbolea za viwandani, na zinakuwa na kiasi kikubwa cha virutubisho vya asili.

Kabla virutubisho vyake havijachukuliwa na mimea, mbolea za asili ni lazima zimeng’enywe kwanza na viumbe hai walioko ardhini na hivyo virutubisho vinaachiliwa taratibu kwa muda mrefu. Hii ina maana kuwa kuna wakati pia vinakuwa havipo, na kwa kiasi kinachohitajika na baadhi ya mimea.

Mbolea za asili zinawezaje kuoza haraka

  • Maandalizi ya shamba, hii husaidia kuongeza hewa ya oksijeni (oxygen) kwenye udongo.
  • Kuongeza nitrojeni, hii husaidia kuongezeka kwa viumbe hai kwenye udongo na kufanya wawe wachangamfu zaidi.
  • Unyevu, maji yanahitajika katika hatua zote za kibiolojia.

Zifuatazo ni mbolea zisizo za asili zilizo zoeleka kutumika katika kilimo hai na madhara yake.

Mbolea zisizo za asili

Mbolea za viwandani hutoa virutubisho moja kwa moja kwenye mimea kwa kiasi kikubwa, zikiwa zimeyeyushwa kwenye maji. Mmea unaweza kuzipata kwa haraka sana. Wakulima wa kilimo hai wana mashaka juu ya utara huu:

  • Mbolea za chumvichumvi hazisaidii kuboresha uhai wa udongo, lakini zinapunguza endapo zitatumika zenyewe bila kuwepo mbolea za asili kwa muda mrefu.
  • Mbolea nyingi zisizo za asili huongeza tindikali (acid) kwenye udongo, na kujenga mazingira yasiyo rafiki kwa mimea na viumbe wengine.
  • Virutubisho vinavyoyeyuka kwenye maji, hasa nitrate zinakuwa rahisi sana kusafirishwa na maji jambo ambalo pia linaweza kusababisha athari kwa mazingira kama vile kuchafua maji yaliyoko chini ya ardhi.
  • Kuwekea mimea mara mbili au tatu ya kiasi kikubwa cha aina fulani ya virutuibisho, inaweza kusababisha kutokuwa na uwiano kwenye mimea jambo linaloweza kusababisha ongezeko la magonjwa na wadudu.

 

 

 

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *