- Kilimo

Zingatia haya kabla ya kuanza kilimo hai

Sambaza chapisho hili

Wakulima wengi wamekuwa wakitamani kufanya uzalishaji kwa misingi ya kilimo hai na hata wengine wakiwa tayari wanazalisha lakini wakikwama kutokana na mambo kadha kama kukosa soko, mazao kuharibika au kukosa elimu sahihi ya uzalishaji kwa misingi ya kilimo hai.

Wakulima wengi wanakata tamaa kwa kushindwa kufikia malengo huku wengine wakiacha kabisa uzalishaji wa kilimo hai.

Ili uweze kuzalisha kwa usahihi na kufaidika na kilimo hai hakikisha unafanya yafuatayo;

 

  • Misingi ya kilimo hai ni ipi?
  • Nitapata wapi malighafi (Mbolea, viuatilifu asili, matandazo, mbegu etc) zinazohitajika?
  • Je, wapi naweza kuuza mazao yangu ya kilimo hai?
  • Naweza kuuza kwa bei gani?
  • Ni kiasi gani ninaweza kuzalisha na kuuza kwa wateja?
  • Ni nani washindani wangu?
  • Nitafanyaje uzalishaji wa kilimo hai?
  • Kuna mkulima au kikundi cha wakulima ambacho kimefanikiwa katika kilimo hai na je, naweza kuungana nao au kujifunza kutoka kwao?

Unapozalisha bidhaa kwa ajili ya kuuza, ni lazima uhakikishe unatambua soko mapema. Hii itakusaidia pia kutambua umbali na namna ya kulifikia soko, gharama za uzalishaji wa bidhaa pamoja na muda wa bidhaa kukaa sokoni.

Fanya majaribio kwa kuzalisha kidogo

Ukishatambua soko la mazao yako ya kilimo hai, jaribu kuanza kulima mazao kidogo katika eneo dogo. Hii itakusaidia kujua kama uendelee kuzalisha kwa uchache au kwa wingi kiasi gani na endapo pia utakosa soko Je, mazao hayo utapeleka wapi? Hapa unaweza kujifunza namna ya kuzalisha bidhaa mbadala yaani kufanya usindikaji.

Panua uzalishaji

Mara baada ya kuona kuwa itafaa kuzalisha na kuuza mazao ya kilimo hai, anza kuzalisha kwa wingi na tekeleza uzalishaji kwa misingi ya kilimo hai pekee. Hii itakusaidia kuwa na soko la uhakika na bidhaa yako kukubalika sokoni.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0717266007

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *