Tukiwa tunaelekea katika msimu wa mvua za vuli, wakulima wengi hupendelea kupanda zao la maharage kwani ni moja kati ya zao kuu nchini Tanzania. Hata hivyo changamoto za uzalishaji wa zao hili hupelekea wakulima kupata mazao hafifu.
Ni ukweli usiopingika zao la maharage ni moja kati ya mazao ya chakula na biashara. Zao hili linazalishwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini, kwa misimu tofauti hasa kulingana na mvua pamoja na hali ya hewa ya eneo husika.
Aidha, kabla ya kuzalisha zao hili kwa misingi ya kilimo hai, mkulima hana budi kufahamu kanuni sahihi kwa ajili ya kufanya uzalishaji bora na wenye tija.
Kanuni za kufuata katika uzalishaji maharage
- Kuchagua eneo la kupanda maharage:
- Joto: Kiasi cha nyuzi joto 12 hadi 32. Joto likiwa chini zaidi au juu zaidi linapunguza ukuaji.
- Mvua: Mvua inayohitajika ni kati ya 400mm hadi 1800mm kwa mwaka zinazonyesha kwa mtawanyiko mzuri.
- Mwinuko: Panda katika maeneo yenye mwinuko wa mita
400-2000 m kutoka usawa wa bahari.
- Mbegu: Uchaguzi wa mbegu sahihi ni muhimu ili kupata mavuno bora. Chagua mbegu zenye soko, mavuno mengi, kinzani/uvumilivu wa magonjwa na wadudu. Mapendekezo ya mbegu yatategemea na ukanda husika.
- Vyanzo vya mbegu bora:
Mbegu bora zinaweza kupatikana kutoka kwa wakulima wanaozalisha mbegu.
- Sehemu ya kupanda maharage:
Panda sehemu zenye udongo usiotuamisha maji na wenye rutuba kwa kilimo cha maharage. Usipande kwenye mteremko mkali, udongo wenye mchanga mwingi na kina kifupi.
- Kutayarisha shamba:
Shamba la maharage linatakiwa liandaliwe vizuri kwa kusafisha, na kuvundika majani ili yaoze na kuwa mbolea.
Baada ya hapo katua shamba vizuri na kulainisha udongo ili uotaji wa mbegu uwe rahisi kisha lima sesa au matuta kufuatana na mwinuko wa ardhi au hali ya maji kutuama.
- Kupanda kwa wakati: Hali ya hewa wakati wa kupanda ni muhimu ili uotaji kuwa mzuri na kupata mimea yenye afya. Mbegu zipandwe kina cha kutosha kupata unyevu na joto kwa mahitaji ya kuotesha. Maharage ni vyema kupandwa kwa kutegemea aina ya mbegu na sehemu husika. Pia hakikisha maharage yanakomaa kuelekea kiangazi au mvua zinaposimama.
- Matumizi mazuri ya mbolea (Aina za mbolea): Kwa maeneo yenye rutuba hafifu mbolea ni muhimu kutumia. Aina na viwango vya mbolea vinavyoshauriwa ni pamoja na;
- Mbolea za asili: Kama mbolea za mifugo au mboji na unashauriwa kusambaza shambani kabla ya kulima. Kiasi: 2000-5000 kilo kwa eka moja.
- Upandaji: Panda kwa nafasi zinazoshuriwa sentimita 50 mstari hadi mstari na sentimita 10 mbegu hadi mbegu (50sm x 10sm). Kina cha inchi 1 hadi 1.5 kinafaa. Mimea ya kutosha shambani inapelekea mavuno mengi.
- Palizi: Palizi inaweza kufanyika kwa kutumia jembe la mkono. Palizi ifanyike angalau mara 1-2 kwa msimu. Wahi palizi ya kwanza ndani ya wiki mbili hadi tatu baada ya maharage kuota na rudia tena kabla ya kuchanua.
- 11. Wadudu na magonjwa: Funza wa maharage ni wadudu wanaoshambulia mimea michanga ya Funza hawa huweza kusababisha uharibifu hadi kufikia asilima 100 kufuatana na hali ya hewa au unyevu kidogo, rutuba kidogo, kuwepo kwa maotea ya aina ya maharage na magogwa kwenye udongo, kurudia kupanda zao la maharage kila msimu na aina ya maharage.
Magonjwa mengine maarufu kama ndui ya maharage, madoa pembe, kutu, magonjwa yanayo sababishwa na bakteria na virusi.
Punguza athari kwa kupanda mbegu safi, aina zinazo vumilia magonjwa na kutunza shamba
Mbinu za kudhibiti magonjwa na wadudu waharibifu wa maharagwe
Njia moja au zaidi kati ya hizi zinaweza kutumika kama kinga:
- Matumizi ya mbegu zenye
- Matumizi sahihi ya mbolea ya asili; mbolea huimarisha afya ya mimea hivyo kuiwezesha kuvumilia na kupambana na madhara yatokanayo na magonjwa na wadudu
- Kupanda kwenye matuta au mashamba yalioinuliwa ili kupunguza kutuama kwa maji lakini pia kusaidia kurutubisha udongo kwenye sehemu zenye muinuko na mvua
- Kupandishia udongo kuzunguka mashina kabla ya maua husaidia mmea kuotesha mizizi bandia kwenye mimea iliyoshambuliwa na Rizoktonia, Fusariam na Funza wa
- Kufukia chini kabisa mabaki ya mimea iliyoshambuliwa wakati wa kuandaa
- Kuacha mabaki ya mazao yaliyopita kuoza kabisa kabla ya kupanda mazao
- Kufanya kilimo cha mzunguko wa mazao ya jamii tofauti kama nafaka kila baada ya miaka miwili au
Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa maandiko yaliyochapishwa kutoka chuo cha ARI Uyole Mbeya. Wasiliana na Mkulima Mbunifu kwa maelekezo zaidi
ttt