TUNAWAKUMBUSHA TENA!
Tarehe 2–3 Septemba 2026 | Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwalimu J.K. Nyerere, Dar es Salaam, Tanzania

Sekta za kilimo, mifugo na usindikaji wa chakula barani Afrika zinaingia katika kipindi kipya cha ukuaji, na mwezi huu wa Septemba, wadau wakubwa wa tasnia hii watakutana chini ya paa moja jijini Dar es Salaam. Maonesho ya 10 ya Africa Agri Expo (AAE 2026), yanayofanyika katika Toleo lake la Jubilei, kwa mara nyingine yataandaliwa pamoja na Maonesho ya 3 ya Future Food, Livestock & Poultry Expo (FLIP 2026), yakileta pamoja mbili kati ya majukwaa muhimu zaidi ya biashara katika ukanda huu, katika tukio moja linalovutia sana.
Aidha, sisi kama Mkulima Mbunifu tutakuwepo kukupa elimu kuhusu kilimo, mifugo, uvuvi, na kilimo ikolojia kwa ujumla. Njoo uzungumze nasi na ujipatie vipeperushi mbalimbali vya elimu kutoka kwetu.

Iwapo wewe ni mkulima, msambazaji, muuzaji, mtaalamu wa biashara ya kilimo, au kiongozi mtunga sera, mwenye kujali maslahi katika mustakabali wa kilimo Afrika Mashariki, hili ni tukio ambalo hupaswi kulikosa.
CHIONDE CHONDE, USIPANGE KUKOSA….
NJOO UKUTANE NA WABOBEVU KATIKA SEKTA MBALIMBALI NA UPATE KUJIONE FURSA MBALIMBALI ZA KIBISHARA




