650
- Kilimo

Parachichi ni tunda lenye faida za lishe na kiuchumi

Sambaza chapisho hili

Parachichi limekuwa tunda mbadala na la kuvutia kwa wakulima wanaopanda miti ya matunda, na kuonyesha uwezo mkubwa kwa wakulima kupata mapato bora.

m

Parachichi ni zao linaloonekana kuwa na faida kubwa hasa kipesa na hata kiafya kwani lina vitamin A, C na mafuta kwa wingi. Uhitaji wake umekuwa kwa kasi sana hapa Tanzania. Hii imetokana na kuwepo kwa kampuni za kusafirisha kupeleka nje ya nchi pamoja na kuwepo na viwanda vya kutengeneza mafuta kutokana na parachichi.

Aina za parachichi

Aina za parachichi zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni kienyeji na kisasa.

Parachichi za kienyeji ni nzuri kulima kwa ajili ya chakula, lakini za kisasa ni nzuri zaidi kulima kwa ajili ya biashara na chakula.

Aina za parachichi za kisasa

Parachichi ya kisasa ni pamoja na hass, fuerte, ndabal, booth, etinger na waisal.

Aina hizi za parachichi hupendwa sana sokoni kwa kuwa zina kiasi kikubwa cha mafuta au siagi.

Hass na Fuerte: Aina hizi za parachichi hukomaa mapema sana. Huchukua miezi sita kukomaa mara baada ya kutoa maua.

Parachichi hizi zina mafuta mengi, lina soko kubwa nan i ndogondogo kiasi cha ukubwa wa gramu 250 hadi 750.

Ndabal: Aina hii ya parachichi ina matunda makubwa ukubwa wa gramu 800 hadi kilogramu 1. Huchelewa kukomaa kwani huchukua miezi 8 kukomaa mara baada ya kutoa maua.

Waisal na Etinger: Aina hizi za parachichi huvumilia ukame na huchukua miezi 4 hadi 5 kukomaa.

650

Kuna aina zingine za parachichi ambazo ni;

Puebla: Aina hii hutumika na wakulima wengi kwa kuwa ina uimara zaidi na matunda yake hayana nyuzinyuzi na ina uwezo mkubwa wa kukabiliana na magonjwa.

Singapore: Hii ni aina mpya ya parichichi ambayo inakuwa kwa haraka sana na kufikia kukomaa katika kipindi cha miezi 15. Inakuwa kwa urefu wa futi 2.

G5 na G6: Aina hizi mbili ni maarufu sana kwa kuwa zinafanya vizuri zaidi katika maeneo ya mwinuko na hata katika maeneo ya tambarare. Aina hizi zinaweza kupandikizwa katika aina nyingine zozote za miparachichi ili kuongeza ubora wa matunda.

Uoteshaji wa mbegu za parachichi

  • Mbegu za parachichi za kisasa mara nyingi hushindwa kumudu magonjwa wakati wa uotaji na wakati mwingine huweza kutokuota hivyo inabidi kupandikiza kwenye pandikizi za kienyeji.
  • Hatua ya kwanza, unahitajika kukusanya mbegu za kienyeji kutoka kwenye miti mama yaani parachichi zilizoomaa na kuiva.
  • Andaa udongo wa kupandia. Udongo huu ni vyema kukusanya kutoka msituni na kuuchanganya na mboji au samadi iliyoiva, majivu, mchanga na maranda au makapi ya mpunga.
  • Katika mchanganyiko huo, uwiano wake ni debe 1 la mchanga, udongo debe 2, mboji debe 2, maranda debe 1 na majivu ⅙ ya mchanganyi wote.
  • Changanya kwa pamoja huku ukinyunyizia maji kidokidogo kisha jaza kwenye viriba vyenye upana wa inchi 4 na urefu wa inchi 6.
  • Otesha mbegu moja moja katika kila kiriba na hakikisha mbegu unayootesha imekauka vizuri na umeondoa maganda.
  • Mbegu hii huchukua wiki moja hadi tatu kuota, na mwezi mmoja mpaka kuwa na uwezo wa kubebesha (ili shina la mche liweze kuwa imara). Hakikisha mche umefikia unene wa kalamu ya risasi na urefu wa futi moja.

Tumia teknologia ya upandikizaji

Upandikizaji hujumuisha aina mbili za mimea. Unachukua mmea mmoja ambao unadhani hauna tija nzuri, na sehemu ya mmea mwingine ambao una ubora zaidi na kupandikiza kwa kukata na kufunga pamoja ili kupata mbegu bora zaidi.

Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati mmea umefikisha unene wa penseli. Kupandikiza kwa kutumia chipukizi lililolingana na mche unaopandikizia ni njia yenye mafanikio zaidi.

Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati ambao mizizi bado ni laini. Pandikizi litakalotumika wakati wa kupandikiza ni lazima lisiwe katika hatua ya ukuaji kwa wakati huo, na ni lazima umbo liwiane na mti linapopandikizwa. Funga vizuri kwa kutumia nailoni ili kuzuia maji yasipotee na kusababisha pandikizi kukauka.

Mapandikizi ni lazima yatokane na aina ya parachichi ambazo zimeboreshwa kama vile hass, fuerte au pueblo. Kwa wale wakulima ambao wana mkataba na Africado, watahitaji kupata mapandikizi kutoka kwenye miti ya hass. Hii ina maanisha kuwa mkulima anayetaka kuanzisha kitalu kwa ajili ya kupandikiza ni lazima apande walau miti 5 ya parachichi aina ya hass au aina nyingine ya kisasa na yenye ubora ili kupata mapandikizi.

Njia ya kupandikiza ina ufanisi zaidi na ni rahisi kuliko kupanda miche upya, kwa kupandikiza inagharimu chini ya asilimia 75, kuliko kupanda miche upya na kuweza kupata aina ambayo inastahimili magonjwa. Wakulima pia wamekuwa na rikodi nzuri ya ongezeko la mavuno kutokana na mimea waliyopandikiza, pamoja na upungufu wa matumizi ya madawa.

Matunzo

Hakikisha unapalilia mara kwa mara ili kuondoa magugu yasiweze kuua miche.

Kama ni wakati wa kiangazi hakikisha unamwagilia maji ya kutosha ili udongo uweze kuwa na unyevu wa kutosha wakati wote.

Upuliziaji wa dawa ni muhimu ili kukinga magnjwa ya ukungu na wadudu kama vile inzi weupe, kimamba wekundu na wengine.

Mara nyingi miparachichi haishambuliwi na wadudu wala magonjwa hivyo upuliziaji unahitajika kufanyika pale panapokuwa na ulazima au kwa kiwango kidogo.

Kila mwaka miti mikubwa na midogo itakapotoa maua, miche nayo itatoa hivyo hakikisha unayaondoa maua hayo.

Mara nyingi mavuno ya miparachi aina za kisasa huanza kukomaa miaka mitatu toka kuanda mche.

Soko

Soko la parachichi kwasasa limekuwa sana, kutokana na upelekaji wa matunda haya nje ya nchi pamoja na usindikaji wa bidhaa zinazotokana na parachichi.

Angalizo: Usioteshe miparachichi kwenye udongo wa mfinyanzi na hakikisha unatumia mbegu zenye ubora.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *