- Kilimo, Udongo

Namna ya kutambua kufanya udongo uwe na afya

Sambaza chapisho hili

Katika sekta ya kilimo, rutuba kwenye udongo ni jambo muhimu la kuzingatia kwani huweza huathiri usalama wa chakula na mazingira.

Kumekuwa na ongezeko kubwa la uhitaji wa chakula duniani  kutoka katika eneo lile lile dogo linalotumika kwa uzalishaji, huku ardhi hiyo ikikabiliwa na madhila kama vile mmomonyoko wa ardhi na ongezeko la wadudu wanaopunguza uzalishaji kila wakati.

Viini vya rutuba ya udongo

Rutuba ya udongo hutengenezwa na vitu vitatu muhimu ambavyo ni uasilia wa kibayolojia, kikemia na kifizikia.

Viumbe hai wana mchango mkubwa sana katika kuendeleza rutuba ya udongo. Njia rahisi ya kutambua biyolojia na ufanyaji kazi wa udongo ni kwa kuangalia uwepo wa nyungunyungu (earthworm).

Kujua muundo wa udongo husaidia kuweka usawa kati ya upitishaji wa hewa safi, umwagiliaji na ushamirishaji wa mizizi. Hili linaweza kufanikiwa kwa kupima udongo ili kufahamu muundo wake.

Pembejeo za kilimo hai pamoja na mbinu za kilimo zinazosaidia katika kuzuia kusumbuliwa kwa udongo na kusawazisha upatikanaji wa viumbe hai zinaweza kutumiwa ili kuimarisha udongo na kulinda ardhi.

Namna ya kutambua rutuba ya udongo

Njia nzuri mojawapo ya kuweza kutambua rutuba ya udongo ni kwa kuangalia kudondoka kwa masazo ya mimea, uwepo wa mende na mashimo yanayoonyesha uwepo wa shughuli za wadudu na harufu.

 

Viashirio vya udongo wenye rutuba

  • Hauwezi kugandamana baada ya kuotesha
  • Una harufu nzuri
  • Hutoa mazao na nyasi zenye afya na ubora.

Faida ya utunzaji wa rutuba ya udongo

Utendaji mzuri wa shughuli mbalimbali za kilimo ambazo husaidia katika uboreshaji na utunzaji wa afya ya udongo hulenga zaidi katika;

  • Kuboresha na kudumisha viumbe hai katika ardhi
  • Kuepusha shughuli za ulimaji zinazoweza kuharibu muundo wa udongo
  • Kuhifadhi udongo kutokana na mmomonyoko na madhara mengine ya uzalishaji
  • Kupitisha madini jumuishi, na kusaidia kuwepo kwa udhibiti wa wadudu na magonjwa
  • Kurekebisha matatizo ya udongo kama ya asiditi na alkaliniti
  • Kurahisisha ufanyaji kazi katika namna mbalimbali
  • Kuhifadhi unyevu kwa ajili ya vipindi vya kiangazi
  • Kuzuia mmomonyoko wa udongo na upotevu wa virutubisho
  • Kusaidia katika upatikanaji wa idadi kubwa ya viumbe hai na wadudu warutubishaji wa udongo

Mfumo wa rutuba ya udongo

Udhibiti wa kibayolojia

Magonjwa yanayotokana na udongo, hasa yale yanayosababishwa na vimelea aina ya pathogens husababisha hasara ya upotevu wa mavuno, jambo linaloelezwa na wakulima kuwa hutokana na matumizi ya viua kuvu.

Hata hivyo, kuendeleza matumizi ya dawa ya kuvu katika mfumo wa kilimo cha aina moja ya mazao husababisha kuongezeka kwa kiasi cha kuvu katika udongo na kuathiri usawa wa utendaji kazi wa udongo.

Aidha, kupitisha mfumo wa pamoja wa kulinda afya ya udongo kwa kutumia bidhaa zenye vimelea vya kuzuia magonjwa ni lazima kuwepo kwa visaidizi vya kukuzia mimea.

Hii inaweza kujumuisha njia za asili za kuongeza nitrojeni kwenye udongo, ili kusaidia kupambana na magonjwa yaliyomo kwenye udongo kama vile fusari na mengineyo ambayo husababisha shina na mizizi kuoza.

Kilimo cha mzunguko

Kupanda mazao kwa mzunguko husaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti wadudu na magonjwa, pamoja na kulinda rutuba ya udongo.

Usimamizi endelevu wa rutuba ya udongo

Upimaji

Ni muhimu kwa wakulima kupima udongo ili kujua kiwango cha ufanyaji kazi pamoja na kuweza kutambua ni kwa kiasi gani virutubisho vya ziada vinahitajika.

Virutubisho hivyo ni pamoja na chokaa, jasi, samadi na mbolea, ambazo husaidia kuwepo kwa uwiano mzuri wa madini yanayohitajika ardhini, kuokoa muda na fedha ambazo kwa namna nyingine zingetumika kwa wingi katika kushughulikia ukuzaji wa mimea.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *