Kama ilivyo ada, Mkulima Mbunifu hutembelea wakulima wanufaika wa jarida la kilimo hai nchini Tanzania. Hivi karibuni, Mkulima Mbunifu ilitembelea kisiwa cha Zanzibar ambapo iliweza kufanya mahojiano na baadhi ya wakulima wa kilimo hai na wanufaika wa jarida la Mkulima Mbunifu Zanzibar.
Katika makala hii tutamuangalia Bi. Salma Hussein Makame, Mkulima wa kilimo hai kutoka kijiji cha Unguja Ukuu, Wilaya ya Kati Mkoa wa kusini Unguja.
Yeye ni mkulima tangu mwaka 2018 ambapo alipata elimu kupitia wadau mbalimbali wa kilimo hai hapa Zanzibar na bara kama UWAMWIMA, TOAM, Milele Foundation na SAT- Morogoro. Kupitia UWAMWIMA nilipokea vijarida vya Mkulima Mbunifu kila mwezi ambapo husoma na kufatilia sana makala hasa za kilimo cha mboga mboga, matunda, utengenezaji wa madawa ya asili.
Bi Salma anasema “Nimekua najifunza mambo mengi kupitia jarida la Mkulima Mbunifu, na nahakikisha kila mwezi nafatilia UWAMWIMA kama yamefika. Napenda sana kusoma hasa kuona wenzetu bara wanavyo tekeleza kilimo hai na kufanikiwa”.
Bi Salma anajishughulisha na kilimo cha mboga mboga na matunda kwaajili ya matumizi nyumbani na pia anafanya biashara. Anaeleza “Mimi ninazalisha mboga za jamii za sukuma wiki, chainizi, kabeji, mchicha, matembele. Kwenye matunda ninazalisha nyanya, ndizi mapasheni na mipapai. Ninazalisha mazao mchanganyiko shambani ili kujipatia kipato cha kuinulia maisha. Miti ya matunda kama mipapai napata tunda, majani natumia kutengenezea dawa na mbolea”.
Bi. Salma anauza mbogamboga kwa watu jirani ambao hufata mboga hizo shambani. Na pia hupeleka sokoni kuuza hasa siku za soko ili kujipatia kipato cha kujikimu na matumizi ya nyumbani.
Bi Salma anaeleza, faida anayoipata huigawanya mara tatu. Kwanza anaweka akiba kwaajili ya matumizi nyumbani, pia kiasi kingine kinamsaidia kuendesha shughuli za shambani kama kuwalipa vibarua wanao msaidia kwani peke yake hawezi. Tatu ana bakiza akiba kwaajili ya matumizi ya kila siku kwa familia nyumbani.
Anakiri Jarida la Mkulima Mbunifu limemsaidia kujifunza mambo ambayo hajawai kuyafahamu kwenye kilimo. Anasema “ Elimu haina mwisho na hususani ile kazi unayo ifanya kwa vitendo inakupa uzoefu wa kuelewa zaidi. Sasa hivi naweza kutengeneza baadhi ya mbolea kupitia jarida la Mkulima mbunifu, pia naongeza mazao kwenye shamba langu kupitia jarida la mkulima mbunifu. Ambapo utakuta nachukua jarida la Mkulima Mbunifu na soma na baadae nakuta vipengele vinavyo ni husu kama mkulima navitumia kuongezea mapato kwenye shamba langu”.
Napenda kilimo hai kwasababu, najali kutunza afya yangu na familia na wateja wangu. Najali kutunza afya ya ardhi yangu ambayo naifanyia kazi, niweze kupata mazao endelevu kila wakati nijipatie kipato. Na kilimo hiki hakina gharama kwani situmii pesa kwenda kutafuta madawa na mbolea. Hii ndio sababu kubwa inivutia kuachana na mfumo wakutumia sumu na madawa yenye athari kwa binadamu na mazingira.
I am Mwanaisha Chilumba age 28. I would like to get more education On veggies farming and ways on how to achieve Veggies farming goals at large . I am in Unguja at Kisauni
Hello Mwanaisha,
Welcome to MkM Platform and am happy to hear well from you and your interest on veggies farming. We have done a lot on veggies may be you tell us exactly which one do you prefer so that i can assist on providing you with a link so that you go through it online. Or you can search them by typing the name plus word Mkulima Mbunifu E.g. Kilimo cha saumu Mkulima Mbunifu.