- Kilimo

Iliki: Mkombozi wa uchumi wa familia

Sambaza chapisho hili

Iliki ni moja kati ya mazao ambayo yanatumika karibia kila siku kwenye matumizi ya nyumbani. Iliki hutumika kama viungo kwenye chakula na pia kama tiba ya magonjwa mbalimbali. Mmea wa iliki ni mfupi na unatoa matunda kwa miaka mingi.

Aina za iliki

Kuna aina mbili za iliki, ambazo ni:

  • Malabar-Aina hii huzaa kwa kutambaa ardhini na matunda yake ni madogo madogo.

Urefu wa mmea wa malabar ni karibia mita 3.

  • Mysore-Aina hii ya matunda yake huzaliwa kwa wima.

Majani yake ni mapana na mmea una urefu zaidi ya mita 3.

 Mazingira na hali ya hewa  

  • Huoteshwa kwenye maeneo yenye mvua 2500mm kwa mwaka.
  • Eneo liwe na kivuli cha wastani.
  • Udongo uwe wenye rutuba ya kutosha na ulio na unyevunyevu wa kutosha.

Kupanda 

Kuna njia mbili za kuotesha iliki.

  1. Kupanda mbegu
  2. Kupanda miche midogo.

Namna ya kufanya

  • Sia mbegu kwenye kitalu.
  • Pandikiza miche shambani ikiwa na umri wa miezi 3-4 au zaidi.
  • Miche iwe yenye ukubwa wa sm 15 au zaidi.
  • Tenganisha miche inayozaliwa kwenye tunguu moja chini ya ardhi na pandikiza shambani.
  • Chimba mashimo sm 60 x 60.
  • Weka miche na fukia kwa udongo taratibu

  Matunzo

  • Baada ya kupanda, weka matandazo kwenye kila shina.
  • Ondoa mashina ya zamani na yalio nyauka.
  • Rekebisha kivuli. Hii inaweza kuwa kwa kukata matawi ya miti na migomba au kupunguza msongamano wa miche ya iliki yenyewe.

Wadudu na magonjwa

Zuia wadudu waaribifu na magonjwa ili kupata mavuno mengi na yenye ubora

Kuoza kwa majani: Dhibiti kwa kunyunyiza dawa zenye morututu kama dithane m-45 

Virus(mosaic virus): Dhibiti kwa kutumia aina inayo vumilia inzi mafuta.

  • Zuia kwa kutumia dawa za kuuwa wadudu insecticides zisizokuwa na madhara kiafya na kwa mazingira. Dawa za asili ni nzuri zaidi endapo zitatumika mapema kabla madhara hayajawa makubwa.

 Kuvuna

Iliki huchukua miaka 3 tangu kupandwa mpaka kuzaa na kuvuna pale unapopanda miche midogo.

Endapo utapanda mbegu huchukua miaka 4-5 mpaka kuvuna. Matunda huvunwa hasa mwezi March na April.

Matundwa huvunwa na kukaushwa kwenye jua.  Kuna uwezekano wa kuvuna kilo 45-120kg za iliki kwa eka ikiwa imekaushwa.

Matumizi

  • Iliki hutumika kama kiungo kwenye chakula.
  • Hutumika kama mchanganyiko kwenye madawa.
  • Hutumika kwenye mafuta na vipodozi.
  • Hutumika kutengeneza vinywaji.
  • Hutumika kwenye vitafunwa vya aina mbalimbali.

Faida ya Iliki kiafya

Kutokana na utafiti usio rasmi uliofanyika miongoni mwa wakulima na watumiaji wa Iliki. Zao hili linasadikika kuwa na faida zifuatazo kiafya;

  • Iliki husaidia kuipa uwezo mzuri figo wa kuondoa taka ndani ya mwili, huku ikisaidia kuweka sawa mfumo wa umeng’enyaji chakula tumboni.
  • Kuondoa kiungulia, gesi tumboni pamoja na kusaidia wenye shida ya kukosa choo kwa muda mrefu.
  • Iliki inauwezo mzuri wa kutibu matatizo ya maambukizi kwenye njia ya mkojo, matatizo ya figo na kibofu cha mkojo, sambamba na kupambana na magonjwa mbalimbali.
  • Iliki pia inauwezo wa kukabilina na hali ya mambukizi ya mafua sambamba na kikohozi, huku ikisifika kwa kuwa na uwezo wa kuimairisha mfumo wa mmengenyo wa chakula pamoja na kuondoa maumivu ya viungo mwilini.

Soko la Iliki

Kama ilivyo kwa viungo vingine, Iliki ina soko kubwa wakati wote, kwani huzalishwa katika baadhi ya maeneo, huku mahitajii yake yakiwa ni makubwa kulingana na idadi ya watu, na matumizi yake.

Iliki iliyotunzwa vizuri

Mara nyingi iliki huuzwa sokoni kwa ajili ya matumizi ya kila siku majumbani katika maandalizi ya milo mbali mbali. Pia Iliki huuzwa katika viwanda vya kuzalishia vinywaji, vipodozi na hata vitafunwa.

 

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

7 maoni juu ya “Iliki: Mkombozi wa uchumi wa familia

  1. Habari,

    Mtandao huu unanufaisha kielimu kwa Mkulima na hata mfugaji

    Ninalo ombi binafsi; ninaomba nitumie Picha yenu ya ILIKI kwenye mtandao wangu,

    1. Habari,karibu mkulima mbunifu na asante kwa kuendele kufuatilia na kusoma makala zetu. Picha tumia tu hakuna tatizo.

        1. Habari,
          Bei zimetofautiana na masoko, hivyo ni muhimu kuangalia masoko ya karibu na wewe yanauzaje

    1. Samahani kwa kuchelewa kujibu swali lako. Mikoa inayolima Iliki ni Morogoro, Mbeya, Kilimanjaro na Tanga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *