Ndizi ya Kitarasa ni moja ya ndizi inayotumika kama chakula cha kitamaduni kwa wachaga waishio katika mkoa wa Kilimanjaro. Aina hii ya ndizi hutumiwa kutengeneza unga wa uji, kutengeneza bia ya kitamaduni na kama mchanganyiko wa chakula cha kitamaduni katika sahani. Hata hivyo, wazalishaji wa kitarasa walipungua, kutokana na mabadiliko ya utamaduni, mtindo wa maisha, upatikanaji duni wa soko na kuanzishwa kwa aina nyinginezo nyingi za ndizi.
Kwa mamia ya miaka, wakulima wamekuwa wakichagua na kuhifadhi aina tofauti za ndizi na ndizi, zote zikiwa na matumizi mahususi ya kitamaduni, manukato na ladha ikiwemo ndizi kitarasa.
Kitarasa ni aina ya ndizi ya kipekee kwani ukikata inatoa utomvu wa njano na ambao hauna ukakasi hata ukila ikiwa mbichi. Ni laini ukipika na ukichelewa kutoa jikoni zitarojeka sana. Utomvu wake ndiyo unaoupa ndizi hii umaarufu na upekee kwani una madini mbalimbali yanayohitajika mwilini mwa mwanadamu.
- Unga wa ndizi kifarasa una vitamen A,B,C
- Madini ya potasiamu, kalsiamu, sodiamu, silicon, fosiforasi, na kloraini.
- Husaidia waathirika wa kisukari cha juu kuvuta hewa ya oksijeni vi
- Huleta matokeo mazuri kwa kupunguza unene (obesity).
- Huponya magonjwa mengi ya tumbo
- Huondoa baridi yabisi (rhemathisim) goita, kifua, magonjwa ya neva na kuvimba miguu.
- Huongeza maziwa kwa akina mama
- Ndizi kitarasa husaidia kuondoa kondo la ng’ombe la nyuma wakati wa kuzaa likishidikana kutoka
Matumizi
Unga wake hutumika kupika uji, ugali, mtori, juice, mkate, maandazi, chapati, na keki na pia ndizi yenyewe huweza kupikwa kama chalari.
Unga wa kitarasa ni maarufu na wagonjwa wengi wa kisukari wanautumia kwa uji ama ugali. Ila Kitarasa inashamnuliwa sana na ugonjwa wa mnyauko! Ndizi yenyewe pia haina ladha kama wenzake ndo maana ikakosa umaarufu uchagani. Ina ukakasi kiasi hivyo ukiipika uwe na viungo vya kutosha. Sasa hivi ina hatari ya kupotea! Nimeipanda huku Dar imeshambuliwa na mnyauko hadi imekufa ingawa nilifanikiwa kula hapo mikungu mitatu