- Kilimo

Fahamu kilimo cha ngolo jinsi kinavyofanyika unufaike

Sambaza chapisho hili

Ngolo ni kilimo cha asili kwa jamii ya wamatengo, ambao ni wakazi wa wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma. Kilimo hiki kinahusisha uchimbaji wa vishimo vyenye mita moja za mraba, na kimo cha sentimeta 40-50.

Aina hii ya kilimo, kinafanyika kwenye maeneo yenye mwinuko mkali. Udongo wa maeneo haya una asili ya ulaini hivyo ni rahisi kutengeneza ngolo.

Hatua za kutengeneza ngolo

Ni muhimu kufahamu hatua za msingi zinazohusika katika aina hii ya kilimo. Kilimo cha ngolo kinahusisha wanaume na wanawake katika hatua tofauti.

  • Hatua ya kwanza wanaume huanza kuandaa shamba kwa kufyeka majani na kuacha yakauke kwa muda wa wiki mbili.
  • Hatua ya pili kukusanya majani na kuyapanga katika muundo wa mraba.
  • Hatua ya tatu wanawake huja kuchimba udongo wakitengeneza vishimo (ngolo), Kufukia yale majani ili yaoze na kuwa mbolea.
  • Hatua ya nne kupanda mbegu kwenye kingo za mashimo na hatua ya tano ni kufukia kwa kuchimba udongo sehemu zilezile ili kukamilisha vishimo vya ngolo.
Kilimo cha ngolo kinafaa sana katika milima au mashamba ya miteremko

 

Mazao yanayooteshwa kwenye ngolo

Katika mashamba ya ngolo, mazao ambayo yanaoteshwa na kustawi kwa wingi ni maharagwe, mahindi, mihogo na ngano. Mazao haya hutegemewa sana na jamii hii ya wamatengo kwa chakula

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *