- Kilimo

Tushirikiane kupata soko la mazao ya kilimo hai

Sambaza chapisho hili

Kwa sasa katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania, ni wazi kuwa shughuli za kilimo hai zimeshika kasi, huku kukiwa na ongezeko la wazalishaji wa bidhaa za kilimo hai.

Ni muhimu kuzalisha bidhaa za kilimo hai kwa wingi na kwa kuzingatia kanuni sahihi

Hili ni jambo jema sana kwa kuwa waswahili wanasema taratibu ndiyo mwenda, na kidogo kidogo hujaza kibaba. Na hapa taratibu tunaona mwanga wa dunia kurudi katika hali yake ya uasili, ya awali isiyo na matumizi ya madawa hatari, huku afya ya binadamu, wanyama na mazingira ikiimaria na kuwa salama zaidi.

Katika hali hiyo, changamoto kubwa imekuwa ni upatikanaji wa soko kwa ajili ya bidhaa hizo za kilimo hai. Hii inatokana na uelewa mdogo wa walaji walio wengi kuhusiana na bidhaa za kilimo hai.

Ili kufikia malengo ya kuwa na dunia salama, hatuna budi kushirikiana kwa kiasi kikubwa na kwa uwezo wetu wote, kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya kilimo hai, pamoja na kusisitiza matumizi ya bidhaa za kilimo hai. Tushirikiane kununua na kutumia bidhaa hai zitakazofanya maisha yetu kuwa salama.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *