Kabla ya kujifunza namna ya kusindika nanaa (mint), ni vyema tukaangalia kwa ufupi kuhusu zao hili na namna ya kuzalisha. Nanaa ni zao la majani ambalo huzalishwa na kutumiwa kama kiungo. Zao hili la viungo ni muhimu kuoteshwa kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha na wenye pH kuanzia kiwango cha 6 hadi 7. Zao hili huoteshwa kwa kutumia mapandikizi au…
Usindikaji
Sindika soya kuongeza matumizi na ubora wake
Soya ni zao mojawapo katika mazao ya jamii ya mikunde ambalo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Morogoro, Rukwa, Lindi, Mbeya, Iringa na Arusha. Zao hili huwa na virutubisho vingi kama vile wanga, protini, mafuta, madini na hata vitamini. Aidha, lina sifa ya kuwa na kiasi kikubwa cha protini kinachofikia hadi asilimia 40. Soya ni zao la muda…
Usindikaji wa karanga kupata mafuta
Karanga hutumika kama kiungo katika mapishi mbalimbali au kukaangwa ili kutumika kama vitafunwa lakini pia kusindikwa ili kupata mafuta, siagi na rojo. Karanga zina virutubisho vingi kama vile; maji asilimia 7, nguvu kilokari 570, protini gramu 23, mafuta gramu 45, wanga gramu 20, kalishamu miligramu 49, chuma miligramu 3.8, patasiamu miligramu 680, vitamini B miligramu 15.5 na vitamini A (I.U…
Kutoka kuzalisha maziwa mpaka kiwanda cha kusindika
Biashara ya maziwa ni biashara maarafu sana katika maeneo ya kanda ya kaskazini mwa Tanzania ambapo kuna wafugaji wengi. Biashara hii imeweza kuwanufaisha wafugaji wengi ikiwa ni miongoni mwa zao la mifugo linalo wasaidia wafugaji kujikwamua kiuchumi. Uzalishaji na uuzaji wa maziwa ni kitega uchumi kizuri ikiwa itafanywa kwa kuzingatia kanuni, taratibu na kuzalishwa katika hali ya usafi. Biashara hii…