Upatikanaji wa mazao bora hutegemea matumizi ya aina na ubora wa mbegu za mazao husika. Baadhi ya wakulima nchini Tanzania wamesahau matumizi ya mbegu za asili na kujikita zaidi katika mbegu za kisasa. Mbegu ni nini? Mbegu ni sehemu ya mmea ambayo mmea mpya unaweza kuota. Kuna makundi makuu mawili ya mbegu ambayo ni; Punje: Kama vile nafaka au mbegu…
Kilimo
Usindikaji wa mafuta ya parachichi nyumbani
Unaweza kusindika na kukamua mafuta ya parachichi nyumbani Parachichi ni moja ya zao la matunda ambalo liko katika kundi la mmea wenye ghala mbili, yaani tunda lake hulizunguka peke linalokuwa ndani. Kitalaamu parachichi huitwa Persea Americana na huweza kusindikwa na kupata mafuta. Namna ya kusindika parachichi kupata mafuta Kuna njia mbalimbali za kutengeneza mafuta kutokana na parachichi lakini mkulima anaweza…
Mnyororo wa Kilimo Ikolojia
Kilimo ikolojia ni mfumo wa ukuzaji wa mimea au mifugo kwa njia jumuishi inayowezesha kufikia ustawi wa kijamii kimahitaji, kimazingira na kiuchumi. Inatafuta kuboresha mwingiliano kati ya mimea, wanyama, binadamu na mazingira. Kupitia mfumo huu wa kilimo ikolojia, jamii inajihakikishia usalama wa chakula na utunzaji wa mazingira. Mfumo huu licha ya kuhakikisha usafi na usalama wa vyakula lakini pia unatusaidia…
Jarida la MkM limenisaidia kufanya kilimo ikolojia kwa faida
Jarida la MkM limenisaidia kufanya kilimo ikolojia kwa faida ‘’Nimekuwa nikifanya kilimo ikolojia toka utotoni kwani wazazi wangu walikuwa wakijishughulisha na kilimo na walitegemea kilimo pekee kwa chakula na biashara, na njia ya uzalishaji ilikuwa ni njia za asili pekee’’. Hayo ni maneno ya Bi. Rehema Joel Mbula (48) mkulima mzalishaji kwa misingi ya kilimo ikolojia na mnufaika wa jarida…
Ulishawahi kujiuliza kwanini tunafanya kilimo?
Kilimo kimekuwepo tangu kale za mababu zetu. Binadamu wa kwanza walipata chakula chao kwenye mazingira yanayowazunguka na kwa juhudi kama uwindaji kabla ya kuanza kulima ardhi, kupanda mazao na kufuga mifugo kama vyanzo vya lishe. Hii ni pamoja na nafaka, mazao ya mizizi, karanga, matunda, nyama, maziwa, na hata mayai. Kilimo kimebadilisha maisha na maisha pia yamebadilisha muundo wa kilimo.…
Lishe ya mbogamboga ni muhimu kwa afya
Mbogamboga ni mojawapo ya chakula bora kwani zikiliwa zenyewe kwa kuchanganya zina viini lishe tosha. Hata hivyo, Mbogamboga zimegawanyika katika makundi kutokana na sehemu ya mmea iliyo muhimu katika chakula cha binadamu na viini lishe vipatikanavyo. Sehemu za mmea wa mbogamboga zinazotumika kama chakula ni pamoja na mizizi, shina, majani, matunda, maua na mbegu. Kazi muhimu za Mbogamboga kwenye chakula…
Zifahamu kanuni za kilimo ikolojia kwa uzalishaji wenye tija na lishe bora
Kilimo ikolojia ni njia ya kilimo inayolenga kuhifadhi mazingira, kuhimiza uendelevu, na kukuza ustawi wa jamii kwa kuzingatia mifumo ya ikolojia na utamaduni wa eneo husika. Ni mfumo ambao unazingatia uhusiano wa karibu kati ya mimea, wanyama, binadamu, na mazingira yao, na kujaribu kuiga mifumo ya asili ili kudumisha bioanuai na kuzuia uharibifu wa mazingira. Kanuni na vipengele 13 vya…
Faida na matumizi ya mbolea ya kijani
Mazao ya mbolea ya kijani ni mazao ambayo yanapandwa ili kuongeza rutuba kwenye udongo. Mazao ya mbolea ya kijani ya jamii ya mikunde (ambazo ni zile zinatengeneza mbolea ya naitrojeni kutoka kwenye naitrojeni iliyopo kwenye hewa) zinaweza kuwapa wakulima wadogo faida nyingi sana ikiwa ni pamoja na: Zinatoa kiasi kikubwa cha naitrojeni kwa ajili ya udongo, Zinaongeza tani nyingi za…
Biashara inahitaji mpango thabiti
Miaka ya hivi karibuni serikali pamoja na wadau wengine wamekuwa na mikakati thabiti ya kuwashawishi wakulima kuweka shughuli zao katika mtazamo wa kibiashara. Waliochukua na kuufanyia kazi ushauri huo kisha kufanya shughuli za kilimo, kitaalamu kwa mtazamo wa kibiashara leo wanapata faida kubwa. Faida hiyo haiji kirahisi. Kuwa na wazo ni aina gani ya kilimo unayoweza kuifanya kibiashara pekee haitoshi.…
Tumbaku kwenye mbogamboga
Tumbaku ni dawa ya asili inayoweza kutumika katika kilimo cha mbogamboga Tumia ugoro au chemsha miche 20 ya tumbaku. Dawa hii inazuia wadudu wanaoshambulia mahindi shambani, wadudu wanaokata miche, kupe, vidukari, viwavi na wengine. Chukua gramu 500 za tumbaku, changanya maji lita nane na uchemshe. Chuja baada ya kupoa, ongeza maji lita nane tena na gramu 60 za sabuni ili…







