a) Kusindika pilipili kavu kupata unga Pilipili kali huumiza macho na pia harufu ikivutwa huleta mkereketo ndani ya pua na kifua wakati wa kusaga ili kupata unga. Inashauriwa kuchukua tahadhari zifuatazo; Vumbi la pilipili kali huumiza macho hivyo inashauriwa kuvaa miwani ya kukinga macho na vumbi hilo wakati wa kusaga au kufungasha. Aidha, mtu anayejishughulisha na kazi ya kuchambua, kusaga…
Kilimo
Mwelekeo wa mvua za vuli (Oktoba – Disemba) na nini wakulima wafanye (Taarifa na TMA)
Uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli kipindi cha Oktoba – Disemba 2024, ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na uvuvi, maliasili, wanyamapori na utalii, nishati na maji, usafirishaji (nchi kavu, kwenye maji na angani), mamlaka za miji, afya pamoja…
Umuhimu wa wataalamu kwa wakulima na wafugaji
Wataalamu wa kilimo na mifugo wamepata mafunzo ili kuendeleza mbinu za kilimo na mifugo kwa lengo la kutoa faida kwa wakulima na wafugaji. Baadhi ya wataalamu wanaweza kuona upungufu fulani au kuona kuwepo kwa mantiki kwenye baadhi ya mbinu za asili ambazo bado zinatumiwa katika uendeshaji wa kilimo na ufugaji na kuweza kuafikiana na wakulima hao juu ya kuziendeleza au…
Kabla ya kuingia shambani kuzalisha andaa mpango biashara
Kila mara wakulima wanashauriwa kuweka kilimo katika mtazamo wa kibiashara. Wakulima wanaochukua na kuufanyia kazi ushauri huo, kisha kufanya shughuli za kilimo kitaalamu na kwa mtazamo wa kibiashara ,wanapata faida. Kuwa na wazo ni aina gani ya kilimo unayoweza kuifanya kibiashara pekee haitoshi. Huo ni mwanzo tu. Ni lazima kukusanya au uwe na pesa/mtaji kwa ajili ya kugharamia shughuli hiyo,…
Mkulima wa kilimo ikolojia na mnufaika wa jarida la Mkulima Mbunifu
David pallangyo (65) ni mkulima anayepatikana kijiji cha Embaseni, wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha. Yeye na mkewe Bi. Elieshi Ayo (60) wamejaliwa kuwa na familia ya watoto 6, kati ya hao 4 ni wa kiume na 2 ni wa kike. Mazao anayoyategemea katika shamba lake ni mahindi, kahawa na ndizi. Pia, ni mfugaji wa ng’ombe wa maziwa. David alianza shughuli…
BEI YA MAZAO MAKUU YA CHAKULA KATIKA MASOKO MBALIMBALI HAPA NCHINI
Kama wewe ni mkulima au mfanya biashara, tafadhali pokea taarifa au mwenendo wa bei za mazao makuu ya chakula katika masoko mbalimbali hapa nchini kwa mujibu wa Wizara ya Viwanda na Biashara. Hii itakusaidia kuuza au kununua mazao kulingana na bei iliyoko sokoni. Bonyeza hapa chini https://www.viwanda.go.tz/uploads/documents/sw-1724870465-Wholesale%20price%2026th%20August,%202024.pdf
Tutunze mazingira na tusichome misitu hovyo
Katika maeneo mengi nchini Tanzania, uharibifu wa mazingira hasa unaotokana na ukataji miti ovyo kwa ajili ya kuchoma mkaa, ujenzi na shughuli za kilimo umekithiri kwa kiasi kikubwa. Jamii nyingi zimekuwa zikifanya hivyo bila kufahamu kuwa umaskini walio nao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa misitu. Imekuwa ni kawaida kwa watu wengi wanaoishi kuzunguka misitu katika maeneo mbalimbali hapa…
Hifadhi nafaka kwa njia sahihi kuepuka upotevu
Ni wazi kuwa wakulima wengine wamevuna nafaka mbalimbali kama vile maharage na mahindi katika msimu huu wa mavuno hivyo wasipokuwa makini na kuhifadhi kwa usahihi mavuno yote yatapotea kwa kuharibiwa na wadudu, panya, au hata ukungu unaotokana na unyevu. Ili kuepukana na hasara ni muhimu kuhakikisha unahifadhi mazao yako katika njia salama kama unavyoshauriwa na Mkulima Mbunifu au wataalamu wa…
JOB VACANCY: INTERN FOR MKULIMA MBUNIFU PROJECT
Mkulima Mbunifu is seeking to recruit suitably qualified intern to support MkM work in support monitoring activities of the project, data management and feedback from users of knowledge products disseminated. Mkulima Mbunifu (MkM) is a farmer information service organization based in Arusha, Tanzania, and implemented since July 2011 with support from Biovision Foundation, Switzerland and Biovision Africa Trust (BvAT), Nairobi,…
Vidokezo muhimu kwa wakulima na wafugaji
Ng’ombe wangu anapata choo kigumu sana na mara nyingine, kinaambatana na ute kama makamasi na damu, huu ni ugonjwa gani, na nasikia kuna dawa za kienyeji zinazotibu! Ni dawa gani, na inaandaliwaje? Msomaji MkM Kuna uwezekano mkubwa kuwa ng’ombe wako anasumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kama ndigana baridi au kitaalamu Anaplasmosis. Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakte- ria ambapo mnyama hujisaidia…








