Shirika la Biovision Africa Trust (BvAT) ambalo ni mshirika wa MkM linaanda kongamao la kujadili maswala ya ikolojia na wakulima Afrika Mashariki. Hii ni fursa nzuri ya wakulima na wadau wa kilimo ikolojia kushirikishana njia na mbinu za kupanua na kusambaza uelewa na habari za mbinu endelevu za uzalishaji. Kongamano hili litafanyika Nairobi, Kenya, tarehe 25-28 mwezi wa Machi mwaka…
Kilimo
Mbolea ya mifupa, kwato na pembe
Napenda kuchangia kipengele cha matumizi ya mbolea za asili toka Jarida la mkulima mbunifu toleo la 3 Novemba 11 na Moduli ya 11. Kusanya mifupa, pembe au kwato kutoka kwenye bucha, hotelini, machinjio, mabandani na nyumbani kwako. Rundika kisha choma moto. Kwa kawaida mifupa huwaka kwa urahisi sana na kwa muda mfupi. Baada ya kuungua, acha mifupa, pembe au kwato…
Usitumie kemikali shambani kwako ni HATARI!
Wakulima wamekuwa wakitumia kemikali kiasi cha kutisha kwenye nyanya kwa ajili ya kudhibiti wadudu. Uzalishaji wa nyanya unaweza kuwa na faida kwa mkulima. Msimu ambao nyanya zinakuwa chache bei hupanda kwa haraka jambo linalomaanisha mkulima anapata faida zaidi. Kwa upande mwingine zao la nyanya ni rahisi sana kushambuliwa na wadudu na magonjwa. Tatizo moja kubwa la kutumia dawa za kudhibiti…
Hakikisha unaweka mipango thabiti katika uzalishaji
Imekuwa ni kawaida kwa wakulima walio wengi kufanya shughuli zao bila kufanya maandalizi thabiti, na bila kuwa na mipango endelevu. Jambo hili ni hatari sana kwa maendeleo, hii ni kwa sababu hautaweza kufanya kazi zako kwa malengo. Utakuwa mtu wa kuchukua kila linalokuja mbele yako, na mwishowe unajikuta haujaweza kufanya jambo la maendeleo na kutokufikia malengo pia. Mwaka umeanza, endapo…
Fahamu kuhusu magonjwa ya maharage na namna ya kudhibiti
Maharagwe hushambuliwa na magonjwa kadhaa shambani, na pia huweza kuharibiwa na wadudu shambani ama wakati wa kuhifadhiwa. Kutu ya Maharagwe Ni ugonjwa unaosababishwa na ukungu na kwa kawaida hushambulia majani, shina na mifuko ya maharagwe. Dalili kuu za ugonjwa huu ni madoa yenye rangi ya kutu yenye unga ambao unaweza kuonekana kwenye majani, shina au vifuko vya mmea. Madoa yanaanza…
Ni muhimu kuhakikisha usalama na kuzuia upotevu wa chakula
Umakini wa uzalishaji huzuia upotevu wa chakula Upotevu wa chakula hutokea katika mnyororo mzima wa uzalishaji, kuanzia shambani hadi usambazaji kwa wauzaji rejareja hadi kwa walaji. Upotevu huo unaweza kusababishwa na ukungu shambani, wadudu, au udhibiti duni wa hali ya hewa; hasara nyingine hutokana na njia za upishi na upotevu wa chakula kwa makusudi. Upotevu wa chakula husababisha hasara kabla…
Faida ya kuzalisha kwa misingi ya kilimo ikolojia
Malengo ya kilimo ni kuzalisha chakula na bidhaa zingine ili kutosheleza mahitaji ya kaya, jamii na nchi kwa ujumla. Kufuatana na hilo, ni vyema kuhakikisha kwamba wakulima wanazalisha chakula chenye virutubisho, safi na salama kwa walaji na wote wanaotumia bidhaa zinazotokana na kilimo. Kilimo pia huchangia ajira na ustawi wa kichumi katika ngazi mbali mbali. Hivyo, tunapopanua kilimo, tunachangia malengo…
Tumia Teknolojia Rahisi Kuboresha Uzalishaji
Teknolojia ifaayo ina sehemu kubwa katika kuboresha mapato ya wakulima kwa kutoa suluhisho na kuongeza uendelevu yanayoendana na mahitaji na masharti mahususi ya wakulima wadogo. Ikiwa wakulima watatumia teknolojia inayofaa basi wanaweza kuongeza kipato chao hasa katika kuongeza thamani mazao yao. Kutokana na hilo, kwa miaka mingi sasa, kumekuwa na jitihada nyingi kwa ajili ya kuleta mabadiliko na ukombozi wa…
Mahitaji ya uzalishaji wa mbogamboga
Mbegu Kwa matokeo mazuri ikiwemo ukuaji mzuri wa mbogamboga na mavuno mengi mkulima anashauriwa kutumia mbegu bora zilizothibitishwa. Mbegu hizo huwa na sifa zifuatazao: Hutoa mavuno mengi ya kiwango bora. Zina uwezo mkubwa wa kuota. Huhimili baadhi ya wadudu na magonjwa. Hukua kwa haraka, kwa usawa na ni imara. Ikolojia ya Eneo Eneo linalofaa kwa uzalishaji wa mbogamboga za majani…
HERI YA MWAKA MPYA WA 2025!!!!!!
Ni matumaini yetu kuwa tumevuka wote salama na tuko tayari kuanza mwaka kwa kishindo na kwa mafanikio makubwa. Mkulima Mbunifu tumejiandaa vyema kuendelea kufikisha elimu kwako na kwa kushirikiana na wewe katika kuhakikisha tunatatua changamoto zote za kilimo na ufugaji na kuhakikisha upatikanaji wa chakula bora na salama huku tukilinda afya zetu, afya za wanyama, afya ya mimea pamoja na…