Vitamini A ni mchanganyiko wa vyakula tofauti pamoja na baadhi ya matunda. Wataalamu wa afya wamekuwa wakisisitiza kila mmoja katika familia ale matunda na mboga za kutosha ilikupata vitamin A ya kutosha katika mlo wake kila siku, ilikuongeza kinga ya mwili, kuongeza uwezo wakufikiri na kupunguza hatari ya magonjwa. Ni kwa namna gani Vitamini A inatufanya tuwe na afya iliyobora?…
Kilimo
Namna ya kutambua kufanya udongo uwe na afya
Katika sekta ya kilimo, rutuba kwenye udongo ni jambo muhimu la kuzingatia kwani huweza huathiri usalama wa chakula na mazingira. Kumekuwa na ongezeko kubwa la uhitaji wa chakula duniani kutoka katika eneo lile lile dogo linalotumika kwa uzalishaji, huku ardhi hiyo ikikabiliwa na madhila kama vile mmomonyoko wa ardhi na ongezeko la wadudu wanaopunguza uzalishaji kila wakati. Viini vya rutuba…
Liki (leek) moja ya mazao ya mboga yasiyoshambuliwa na magonjwa
Ni vyema kuchagua aina ya mazao ambayo hayana gharama kubwa kuzalisha, wakati huo huo yakiwa na faidi kubwa. Kwa mtindo huo utaweza kupata faida ya kutosha. Liki ni moja ya mazao ya mbogamboga, ambayo yanapata umaarufu mkubwa nchini Tanzania, kutokana na kuzalishwa katika maeneo mengi, na kuwa na soko la uhakika. Zao hili ni moja kati ya mazao ya mboga…
Kilimo mseto na utunzaji wa mazingira
Mara nyingi wafugaji wa mbuzi na hata wale wa wanyama wengine huendesha pia shughuli za kilimo. Katika mashamba yao ya mazao huotesha pia mimea ya aina nyingine, hii ikiwa ni pamoja na miti. Kilimo mseto ni mfumo wa kilimo wa kuchanganya miti na mazao katika shamba moja. Miti sahihi kwa kilimo mseto humnufaisha mfugaji kwa njia nyingi. Miti hiyo huweza…
Fahamu dawa za asili kudhibiti magonjwa na wadudu katika kilimo ikolojia
Dawa ya kufukuza wadudu Dawa hii hutumika kudhibiti wadudu kama nzi weupe katika mipapai, nyanya, tikiti, vitunguu, mboga-mboga na matunda. Mahitaji muhimu Mchele kilo 1 Maji lita 1 Chombo cha ujazo wa lita 2. Jinsi yakutengeneza Changanya mchele na maji katika chombo kisafi chenye mfuniko wakubana. Vundika kwa siku saba, baada siku saba itakuwa tayari kwa matumizi. Matumizi Chukua kiasi…
Maharagwe ni chanzo cha protini na madini kwa watoto
Lishe ni sehemu muhimu ya afya na maendeleo. Lishe bora inahusisha kuboreshwa kwa afya ya watoto wachanga ili kuwawezehsa kukua vyema, kujenga kinga imara zaidi, kupunguza hatari ndogo ya magonjwa na kuwa na maisha marefu. Watoto wenye afya bora hujifunza mambo kwa haraka na kufanya vyema shuleni. Wanapokuwa watu wazima wana nguvu na uwezo wakujitengenezea nafasi ya kuvunja mzunguko wa…
Yafahamu magonjwa ya mimea ili kuyadhibiti
Mkakati mzuri kwa wakulima wanaozingatia ikolojia ni kujifunza na kuelewa sababu ya magonjwa, athari zake ili kuweza kukabiliana nayo. Hii inasaidia kulinda mazao ya mimea, kudumisha usalama wa uzalishaji wa chakula. Kwa kawaida, ni ngumu kuzuia ama kurekebisha tatizo ikiwa haujaelewa tatizo lenyewe. Ndio maana wakulima wanashauriwa kuwa makini shamba-ni kutambua kwa haraka uvamizi wa wadudu na pia magonjwa. Maana…
Ubunifu wa kilimo hai hushamirisha ujasiriamali
Hivi sasa nchini wakulima wanazalisha matunda na mbogamboga kwa wingi na katika maeneo mengi. Hii ni kwa sababu wanatambua jukumu lao katika kuongeza mapato yao ya kilimo na ustawi wa familia kama lengo la shughuli zao za kilimo. Hivyo ni muhimu wazalishaji kuhakikisha hawakosi mifumo mizuru kwa ajili ya mazao yao. Ni muhimu wakulima kuhakikisha kunakuwepo na mifumo mizuri ya…
Ushuhuda kutoka kwa msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu
Kama ilivyo ada, Mkulima Mbunifu tumeendelea kuwatembelea wakulima na wanufaika wa jarida hili kufahamu ni kwa namna gani elimu wanayoipata kupitia makala za kila mwezi zimeendelea kuleta chachu katika shughuli zao za kilimo na hata kuweza kuwabadilisha kimaisha. Bi. Esther Kitomari ni miongoni mwa wanufaika wa jarida la MkM na anaeleza kuwa amejifunza mengi kupitia makala zinazochapishwa kila mwezi hasa…
Umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira
Utunzaji mahiri wa mazingira na vyanzo vya maji, maisha ya kila kiumbe hai yatakuwa hatarini. Hii ni kwa sababu mazingira salama ndiyo chanzo cha uhai kwa viumbe vyote. Ni dhahiri kuwa wote tunafahamu umuhimu wa maji katika kuendesha maisha ya wanadamu, wanyama na viumbe wengine. Ni ukweli usiopingika kuwa viumbe vyote vinategemea maji ili viweze kuishi. Viumbe hai hutegemeana na…









