Kilimo Biashara

- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Kutuhusu, Masoko

MAONYESHO YA WAKULIMA NANENANE, EWE MKULIMA, MFUGAJI NA MJASIRIAMALI VIPI UMEJIANDAAJE?

“Hayawi hayawi sasa yamekuwa”. Kama ilivyo ada mwezi wa nane, huwa ni mwezi wenye shughuli nyingi zinazohusiana na kilimo, ufugaji, uvuvi wasindikaji na hata kilimo biashara tangu mwanzoni kabisa mwa mwezi hadi katikati ya mwezi.  Wakulima, wafugaji na wadau wengine hupata fursa ya kukutana katika maeneo mbalilmbali ili kuonesha kazi zao pamoja na kushirikishana uzoefu katika suala zima la kilimo…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Kutuhusu, Mazingira

Wakulima vinara wa MkM ni mabalozi wa kilimo endelevu

Nchini Tanzania, kilimo si kazi tu, ni sehemu ya maisha ya kila siku. Kilimo kinatoa ajira kwa takribani asilimia 80 ya Watanzania na kuchangia takribani asilimia 30 ya pato la taifa. Kiasi kikubwa cha chakula chetu kinazalishwa na wakulima wadogo. Hata hivyo, licha ya mchango wao mkubwa, wakulima hawa hukumbwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na udongo kupoteza rutuba,…

Soma Zaidi

- Kilimo, Kilimo Biashara

Zingatia afya ya mmea ili kupata mapato mengi

Mara nyingi wakulima wanapuuza maswala yanayohusiana na nafya ya mimea na kupata hasara kubwa. Ikiwa mkulima hatawekeza muda na rasilimali, atakuwa na mimea iliyodhoofika. Ni nia ya kila mkulima kuwa na mimea yenye nguvu na afya, na yenye uwezo wa kutoa mapato ya hali ya juu. Ni lazima kuwa makini na kuzingatia mbinu zitakazowezesha kufikia lengo hili. Hivyo, swala zima…

Soma Zaidi

- Kilimo, Kilimo Biashara, Udongo

Unaweza kutengeneza mbolea ya mboji kwa njia rahisi

Zipo aina nyingi za takataka zin-azoweza kutumika kwa ajili ya kuzalisha mbolea ya mboji kama vile mabaki ya malisho, unga wa maranda unaotokana na shughuli za useremala, majivu na masalia ya ziada baada ya kuvuna mazao shambani. Kwa kutengeneza mboji, kiasi cha mbolea kitakachopelekwa shambani kitaongezeka kwani samadi itachanganywa na takataka zingine na kuozeshwa. Ni jambo zuri zaidi kama mkulima…

Soma Zaidi

- Kilimo, Kilimo Biashara

Unaweza kukausha karoti na kusaga kwa matumizi ya baadaye

Imezoeleka kuwa karoti ni moja ya kiungo maarufu cha chakula, ambacho mara nyingi kinatumika kikiwa kibichi, na mara nyingi hakihifadhiwi kwa muda mrefu. Tofauti na dhana hii, karoti inaweza kusagwa na kuwa unga, ambao unaweza pia kutumika kama chakula. Utayarishaji Osha karoti kwa kutumia maji ya moto hadi zitakate. Katakata vipande vidogo vidogo. Kausha kwenye kikaushio cha sola ili kulinda…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Masoko

Tengeneza unga wa mbegu za parachichi na tumia kwa afya

Unga wa mbegu za parachichi Parachichi ni moja ya matunda maarufu duniani kote. Tunda hili hutumika kwa shughuli mbalimbali, kama vile kuliwa kama tunda, utengenezaji wa mafuta ya kula, vipodozi, n.k. Pia, matawi ya mparachichi yanaweza kutumika kama malisho kwa mifugo, huku mti wake ukitumika kama kuni au hata magogo ya kujengea. Hivi karibuni imegundulika kuwa mbegu za parachichi zina…

Soma Zaidi

- Kilimo, Kilimo Biashara, Mazingira, Udongo

Mvua zinaelekea ukingoni: Panda miti kwa ajili ya mazingira

Kwa mara nyingine tena, wakulima katika maeneo mbalimbali hapa nchini, wanapanda mazao na hata wengine kukazana kufanya palizi ili kutumia mvua ambazo zimenyesha sehemu mbalimbali. Mbali na kupanda mazao, shughuli nyingine muhimu ambayo wakulima wanaweza kujihusisha nayo katika msimu huu wa mvua ni upandaji wa miti. Ni jukumu la kila mkulima kuhakikisha kuwa shamba lake lina miti mipya kila mwaka.…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara

Mazao ya chakula na lishe kamili ni muhimu kwa mkulima

MkM kwenye mtandao wafugaji kwa miaka kadhaa wamekuwa wakifuga kimazoea, bila kuzingatia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wenye tija. Hali hiyo imekuwa ikisababisha kiasi Tanzania ni nchi yenye uwezo wa kuzalisha mazao mengi ya chakula na ya biashara. Hii ni kutokana na hali ya hewa nzuri pamoja na udongo wenye rutuba ya asili unaowezesha mazao hayo kukua na kufanya vizuri katika…

Soma Zaidi