Ufugaji wa samaki umeendelea kukua hata katika maeneo ambayo hakuna ziwa, bahari, bwana na kusaidia jamii kujipatia kipato kinachokidhi mahitaji muhimu, na hata kufanya maendeleo binafsi. Mafanikio ya ufugaji wa Samaki ni kutokana na uhakika mkubwa wa soko.

Katika Makala hii Mkulima Mbunifu inakuletea Ufugaji mesto wa Kuku, Samaki na uzalishaji wa mboga katika mbinu rahisi.
Ufugaji wa mesto ni nini
Ufugaji wa mseto ni ufugaji unaohusisha shughuli zaidi ya moja na kufanya mfumo wa kutegemeana kwenye uzalishaji. Ufugaji huu unahusisha bwawa la samaki, banda la kuku na bustani ya mbogamboga, mfumo huu hufanya mzunguko wa maji ambayo mbolea yake huelekezwa sehemu iliopandwa mazao.
Usiache kufuatilia jarida letu lijalo kwa maelezo ya kina………….




