- Kilimo, Usindikaji

Usindikaji wa mafuta ya parachichi nyumbani

Unaweza kusindika na kukamua mafuta ya parachichi nyumbani Parachichi ni moja ya zao la matunda ambalo liko katika kundi la mmea wenye ghala mbili, yaani tunda lake hulizunguka peke linalokuwa ndani. Kitalaamu parachichi huitwa Persea Americana na huweza kusindikwa na kupata mafuta. Namna ya kusindika parachichi kupata mafuta Kuna njia mbalimbali za kutengeneza mafuta kutokana na parachichi lakini mkulima anaweza…

Soma Zaidi

- Kilimo

Mnyororo wa Kilimo Ikolojia

Kilimo ikolojia ni mfumo wa ukuzaji wa mimea au mifugo kwa njia jumuishi inayowezesha kufikia ustawi wa kijamii kimahitaji, kimazingira na kiuchumi. Inatafuta kuboresha mwingiliano kati ya mimea, wanyama, binadamu na mazingira. Kupitia mfumo huu wa kilimo ikolojia, jamii inajihakikishia usalama wa chakula na utunzaji wa mazingira. Mfumo huu licha ya kuhakikisha usafi na usalama wa vyakula lakini pia unatusaidia…

Soma Zaidi

- Mifugo

Baadhi ya lishe ya vyakula kwa ng’ombe wa maziwa

Ng’ombe wa maziwa anahitajika kulishwa aina ya vyakula vinavyoweza kuupatia mwili wake viinilishe vinavyohitajika kwa ajili ya ukuaji, nguvu, uzazi, pamoja na hifadhi ya viinilishe kama mafuta, protini, madini na majimaji. Ng’ombe huhitaji viinilishe kwa ajili ya kutosheleza mambo yafuatayo; Kuufanya mwili udumu katika hali yake ya kawaida, na kuweza kumudu mambo kadhaa muhimu kufanyika kwa ajili ya kudumisha uhai…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Mifugo

Jarida la MkM limenisaidia kufanya kilimo ikolojia kwa faida

Jarida la MkM limenisaidia kufanya kilimo ikolojia kwa faida ‘’Nimekuwa nikifanya kilimo ikolojia toka utotoni kwani wazazi wangu walikuwa wakijishughulisha na kilimo na walitegemea kilimo pekee kwa chakula na biashara, na njia ya uzalishaji ilikuwa ni njia za asili pekee’’. Hayo ni maneno ya Bi. Rehema Joel Mbula (48) mkulima mzalishaji kwa misingi ya kilimo ikolojia na mnufaika wa jarida…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Mazingira, Mifugo

Ulishawahi kujiuliza kwanini tunafanya kilimo?

Kilimo kimekuwepo tangu kale za mababu zetu. Binadamu wa kwanza walipata chakula chao kwenye mazingira yanayowazunguka na kwa juhudi kama uwindaji kabla ya kuanza kulima ardhi, kupanda mazao na kufuga mifugo kama vyanzo vya lishe. Hii ni pamoja na nafaka, mazao ya mizizi, karanga, matunda, nyama, maziwa, na hata mayai. Kilimo kimebadilisha maisha na maisha pia yamebadilisha muundo wa kilimo.…

Soma Zaidi

- Kilimo

Lishe ya mbogamboga ni muhimu kwa afya

Mbogamboga ni mojawapo ya chakula bora kwani zikiliwa zenyewe kwa kuchanganya zina viini lishe tosha. Hata hivyo, Mbogamboga zimegawanyika katika makundi kutokana na sehemu ya mmea iliyo muhimu katika chakula cha binadamu na viini lishe vipatikanavyo. Sehemu za mmea wa mbogamboga zinazotumika kama chakula ni pamoja na mizizi, shina, majani, matunda, maua na mbegu. Kazi muhimu za Mbogamboga kwenye chakula…

Soma Zaidi

- Kilimo, Udongo

Zifahamu kanuni za kilimo ikolojia kwa uzalishaji wenye tija na lishe bora

Kilimo ikolojia ni njia ya kilimo inayolenga kuhifadhi mazingira, kuhimiza uendelevu, na kukuza ustawi wa jamii kwa kuzingatia mifumo ya ikolojia na utamaduni wa eneo husika. Ni mfumo ambao unazingatia uhusiano wa karibu kati ya mimea, wanyama, binadamu, na mazingira yao, na kujaribu kuiga mifumo ya asili ili kudumisha bioanuai na kuzuia uharibifu wa mazingira. Kanuni na vipengele 13 vya…

Soma Zaidi

- Mifugo

Fahamu mbinu za kuongeza thamani nyama

Safari ya kuongeza thamani nyama ya mifugo huanzia shambani kwa usimamizi wa ufugaji na uzalishaji. Lishe bora ni muhimu kwa wa ufugaji wa mifugo wa nyama, hivyo, nyama nzuri huanza na lishe bora. Malisho ya hali ya juu yasiyokuwa na vimelea vinavyoweza kusababisha magonjwa na kemikali hatari yanakidhi mahitaji ya lishe ya mnyama. Hii itahakikisha mnyama anapochinjwa anatoa nyama laini…

Soma Zaidi

- Kilimo

Faida na matumizi ya mbolea ya kijani

Mazao ya mbolea ya kijani ni mazao ambayo yanapandwa ili kuongeza rutuba kwenye udongo. Mazao ya mbolea ya kijani ya jamii ya mikunde (ambazo ni zile zinatengeneza mbolea ya naitrojeni kutoka kwenye naitrojeni iliyopo kwenye hewa) zinaweza kuwapa wakulima wadogo faida nyingi sana ikiwa ni pamoja na: Zinatoa kiasi kikubwa cha naitrojeni kwa ajili ya udongo, Zinaongeza tani nyingi za…

Soma Zaidi

- Kilimo

Biashara inahitaji mpango thabiti

Miaka ya hivi karibuni serikali pamoja na wadau wengine wamekuwa na mikakati thabiti ya kuwashawishi wakulima kuweka shughuli zao katika mtazamo wa kibiashara. Waliochukua na kuufanyia kazi ushauri huo kisha kufanya shughuli za kilimo, kitaalamu kwa mtazamo wa kibiashara leo wanapata faida kubwa. Faida hiyo haiji kirahisi. Kuwa na wazo ni aina gani ya kilimo unayoweza kuifanya kibiashara pekee haitoshi.…

Soma Zaidi