Katika jamii yetu, watu huchukulia kuwa boga ni chakula cha watu masikini ambao hawana namna ya kupata chakula kizuri. Hata badhi ya wakulima hawakubali kujiingiza katika kilimo cha zao hili. Ukweli ni kwamba, hili ni zao ambalo lina manufaa makubwa sana hasa kwa afya ya binadamu. Hii ni kwa sabababu tunda la boga lina kiasi kikubwa cha kalishamu. Boga ni…
Ikiwa bado tuko kwenye wiki siku ya nyuki, fahamu wadudu wanao athiri uzalishaji wa asali
Siafu Siafu ni miongoni mwa wadudu wanaoshambulia nyuki wanaozalisha asali. Ni wadudu wapole wasiokuwa na shida lakini huvamia mzinga na kuwauwa nyuki. Kutokana na uharibifu huo, humuumiza na kumvunja moyo mfugaji, na mara nyingine wanaweza kuuma na kusababisha maumivu. Kuweka mizinga sehemu yenye siafu inaweza kusababisha utunzaji kuwa mgumu. Kukiwa na kundi dhaifu la nyuki linaweza kusababisha nyuki kuondoka, na…
Mvua zinaelekea ukingoni: Panda miti kwa ajili ya mazingira
Kwa mara nyingine tena, wakulima katika maeneo mbalimbali hapa nchini, wanapanda mazao na hata wengine kukazana kufanya palizi ili kutumia mvua ambazo zimenyesha sehemu mbalimbali. Mbali na kupanda mazao, shughuli nyingine muhimu ambayo wakulima wanaweza kujihusisha nayo katika msimu huu wa mvua ni upandaji wa miti. Ni jukumu la kila mkulima kuhakikisha kuwa shamba lake lina miti mipya kila mwaka.…
Mazao ya chakula na lishe kamili ni muhimu kwa mkulima
MkM kwenye mtandao wafugaji kwa miaka kadhaa wamekuwa wakifuga kimazoea, bila kuzingatia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wenye tija. Hali hiyo imekuwa ikisababisha kiasi Tanzania ni nchi yenye uwezo wa kuzalisha mazao mengi ya chakula na ya biashara. Hii ni kutokana na hali ya hewa nzuri pamoja na udongo wenye rutuba ya asili unaowezesha mazao hayo kukua na kufanya vizuri katika…
Ni hatari kumfunga mbuzi kamba shingoni
Ni dhahiri kuwa wafugaji wengi wana bidii sana na kuwa na matumaini makubwa kutokana na kazi zao. Hari ya kuwa na uzalishaji mzuri kutokana na mifugo yao pia ni dhahiri. Pamoja na hari hiyo, wafugaji wengi wamekuwa hawazingatii kanuni bora za ufugaji na utunzaji wa mifugo yao. Mbuzi wa aina zote wawe wa kisasa au kienyeji wana tabia ya kupenda…
Fahamu ukubwa wa soko la bidhaa za kilimo hai
Historia inaonesha miaka ya zamani kilimo kilikuwa kinafanyika kupitia mbegu za mkulima mwenyewe. Hali hiyo ilitokea kutokana na utaratibu au utamaduni ambao wakulima walirithi kwa mababu kuwa mbegu, mbolea na viuatilifu vya msimu ujayo vinatoka shambani na si kwingineko. Ujio wa mapinduzi ya viwanda duniani unatajwa kuwa ulikuja na faida na hasara zake ambapo moja ya sekta ambayo imepata hasara…
Msimu wa palizi kwa zao la mahindi: Nini wapaswa kufahamu?
Mahindi ni zao muhimu la chakula, na ni aina ya nafaka inayotumiwa kwa wingi kama chakula, hususani katika mataifa ya Afrika, lakini pia limekuwa likitumika katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara. Mahindi ni chakula cha matumizi ya nyumbani kwa idadi ya watu inayokadiriwa kuwa asilimia 50. Ni chanzo muhimu cha madini cha kuongeza nguvu mwilini, protini, madini ya…
Matumizi ya mabaki ya mimea na wanyama katika kurutubisha udongo na kupelekea uzalishaji bora wa mazao
Je, unafahamu kuwa unatakiwa kujua sifa za udongo ulio katika shamba lako na changamoto zake? Je, udongo una upungufu wa naitrojeni? Je, una upungufu wa fosiforasi? Je, kuna uwepo wa mabaki ya miti au wanyama ya kutosha? Ikiwezekana, udongo huo upimwe na mtaalamu au afisa kilimo ili kuonyesha kwa usahihi udongo una mapungufu ya virutubishi vipi na nini kifanyike ili…
Rutuba ya udongo ndiyo msingi wa kilimo hai
Kwa muda mrefu sasa tumekuwa mstari wa mbele katika kuzungumzia na kuhimiza uzalishaji kwa misingi ya kilimo hai, ikiwa ni moja ya nguzo za kilimo endelevu. Katika makala zote zilizochapishwa katika jarida hili pamoja na machapisho mengine yanayotolewa na Mkulima Mbunifu, tumehimiza pia matumizi sahihi ya dawa za asili na mbolea za asili. Hii inatokana na ukweli kwamba, huwezi kusema…
Mnyororo wa ongezeko la thamani utapunguza manung’uniko kwa wakulima na wafugaji
Sera ya soko huria iliyoanza kutekelezwa toka miaka ya 1990 imefungua fursa kwa wawekezaji kuwekeza kwa wingi kwenye maeneo mbali mbali ya kibiashara. Kwa muda mrefu, Kilimo kimewavuta wawekezaji ambao wamekuwa wakijishughulisha na mashamba makubwa ili kukidhi madhumuni ya biashara ya kuzalisha kwa wingi kupunguza gharama ya kuzalisha kwa kiasi kidogo. Pamoja na kutekelezwa kwa makubaliano baina ya wawekezaji na…