- Binadamu, Kilimo

Kemikali huingia mwilini kwa njia mbalimbali

Sambaza chapisho hili

Kwa muda mrefu wakulima walio wengi wamekuwa wakitumia madawa ya kemikali kwa matumizi tofauti, bila kufahamu kuwa wao pia wanaathiriwa na madawa hayo. Dawa hizo huingia mwilini kwa njia mbalimbali.

Ni muhimu kwa mkulima kuelewa vyema jinsi ya kujikinga kutokana na madhara ya madawa ya kuangamiza wadudu, hii ni pamoja na kuacha matumizi ya madawa yenye madhara na namna nzuri ya kujikinga yasiingie mwilini.

Zipo njia mbalimbali ambazo madawa hayo yanaweza kuingia mwilini na kusababisha madhara makubwa, ingawa madawa hayo yanaweza kuingia kwa urahisi kwa njia tatu ambazo ni; kwa kuvuta pumzi, dawa kupitia puani na mdomoni na kufikia mapafu.

Katika shughuli nyingi za kutumia madawa ya kuangamiza wadudu waharibifu madhara hutokana na kupenya kwenye ngozi pamoja na kula.

Hii ni kutokana na dawa kumwagika au wakati wa kunyunyizia kugusana na ngozi, kwa hivyo jambo linalotiliwa maanani katika muongozo huu ni namna ya kuepuka dawa isishike ngozi yako.

Kupitia kwenye ngozi

Madhara kutokana na kupumua huzuka kwa kuwa madawa mengine hurushwa kwa urahisi hewani au njia inayotumika kunyunyiza madawa ya majimaji na ya unga kutoa chembechembe ndogo sana ambazo hufikia sehemu ya kupumua.

 

Hata kama siyo mara nyingi dawa hupenya mwilini, kupitia mdomoni, wakati mwingi madawa ya kuwaangamiza wadudu yanapotumika kuna maelezo kuhusu namna ya kujiepusha kupata madhara kwa njia hii.

Madawa yenye nguvu ni hatari zaidi

Unapaswa kuchukua tahadhari kubwa ikiwa ni pamoja na kuepuka matumizi ya madawa yenye nguvu. Ni muhimu sana kukinga mwili mzima (hasa mikono na uso) yasigusane kabisa na mwili wako. Ni rahisi sana kupata madhara yanayotokana na madawa ya kemikali wakati wa;

  • Kufungwa pakiti zenye madawa ya kuangamiza wadudu
  • Kumimina
  • Kupima
  • Kukoroga
  • Kutumia madawa ambayo yanapendekezwa kwa kiwango kidogo
  • Kusafisha dawa iliyomwagika chini
  • Kutupa ovyo pakiti ambazo zilikuwa na dawa za kuwaangamiza wadudu

Ni muhimu kujiepusha na matumizi ya dawa hizo au kujipatia kinga ya kutosha hasa mikono na miguu ili kupunguza hatari ya kumwagikiwa na dawa. Inapotokea kuwa katika mazingira zinazotumika dawa hizoni muhimu kufunika kichwa, uso na mabega.

Muda utakaotumia dawa

Matumizi ya muda mrefu ya madawa ya kemikali ni hatari zaidi kwa afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira. Kwa kadri dawa hizo zinavyotumika, ndivyo tahadhari kubwa zaidi inavyopaswa kuchukuliwa.

Usafi

Katika mazingira yanapotumika madawa ya kuangamiza wadudu, ni muhimu sana kuzingatia kanuni za usafi kwa umakini hasa kwenye sehemu za mwili zilizoachwa tupu hasa kazi zinapomalizika na kabla ya kula chochote.

Kama ilivyo desturi hakikisha kuwa mavazi na vifaa vyote vilivyotumika au kuwa katika mazingira zilipotumika dawa, v i n a s a f i s h wa au kuhifadhiwa katika sehemu ambayo haviwezi kusababisha madhara kwa afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *