Ng’ombe ni mifugo ambayo inategemewa sana na wananchi walio wengi hapa nchini. Kuna aina tatu za ng’ombe wafugwao hapa nchini ambayo ni ng’ombe wa kisasa, kienyeji, na machotara.
Zifuatazo ni faida zipatikanazo na ufugaji wa ng’ombe
- Chakula kama vile maziwa na nyama
- Mbolea
- Ngozi ambayo hutumika kama malighafi kutengeneza, viatu, mikanda, mikoba, nguo na vitanda
- Kujipatia pesa, pia ni akiba
- Ufahari na huongeza heshima kwa baadhi ya makabila.
- Kupata mapambo kama pembe
Uthibiti madhubuti wa magonjwa mbalimbali
Ili ng’ombe akue vizuri, akupe maziwa mengi na awe na afya nzuri zingatia yafuatayo;
- Uchaguzi wa ng’ombe mzuri wa kufuga
- Malisho mazuri tangia akiwa ndama
- Banda zuri
Chakula cha ng’ombe
Chakula ni kitu muhimu kwa mifugo yote. Ulishaji wa ng’ombe wa maziwa na wengine huanzia toka anapozaliwa (ndama) na ndipo atakapo kuwa na mafanikio mazuri katika uzalishaji.
Ndama anapozaliwa tu anahitaji kupata maziwa ya kwanza (colostrum) kwa muda usiopungua siku tatu mfululizo.
Maziwa haya humsaidia kujikinga na magonjwa na pia humpatia ndama virutubisho vya kutosha. Baada ya hapo ndama aendelee kunywa maziwa ya mama mpaka atakapofikia mwezi mmoja, aanze kupatiwa chakula cha ziada (pumba ya mahindi iliyochanganywa na mashudu pamoja na majani mabichi yaliyokatwa katwa vipande vidogo vidogo).
Ndama akifikia umri kati ya miezi miwili na sita unaweza kumuachisha kunyonya, na anatakiwa apatiwe chakula chenye virutubisho sawa na maziwa ya mama.
Kwa mfano apatiwe pumba za mahindi zilizochanganywa na mashudu na majanimabichi (apatiwe wakati wote).
Ngombe jike wa kisasa hufikia umri wa kupandwa akiwa na mwaka mmoja na nusu. Ng’ ombe atakapokuwa na mimba ya miezi 7 kama alikuwa anakamuliwa anatakiwa kukaushwa na kupatiwa chakula chenye virutubisho zaidi.
Nyumba ya ng’ombe
Nyumba ni muhimu katika ufugaji wa ng’ombe. Tunashauriwa kuwahifadhi ng’ombe katika banda lenye hewa ya kutosha, lisilo na joto kali, lisilopitisha maji ya mvua na liwe lenye nafasi ya kutosha.
Pia banda la ng’ombe liwe na sakafu yenye mteremko kidogo kurahisisha usafi wa banda na kuzuia kutuama kwa maji na mkojo.
Nyumba ya ng’ombe inatakiwa iwe safi wakati wowote ili kuzuia magonjwa mbalimbali.
Naomba kuuliza Kama Kuna mtu anauza molasses nipo Mbeya kyela
0620355983
tnschisunga@gmail.com
Nimejifunza vizuri ila tuomba mtujuze zaidi juu ya ufugaji wa ng’ombe
Habar, Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa swali lako.
Unaposema juu yaufugaji wa ng’ombe ni kipengele gani unahitaji kujifunza kwa maana kupitia makala hii tumeandika dondoo muhimu za ufugaji bora wa ng’ombe
Je ngombe wakisasa niainagani yakufuga nzuri
Habari, karibu Mkulima Mbunifu.
Unamaanisha ng’ombe wa maziwa? Fuga Friesian au Ayrshire
Ni vyema ukiweka picha na aina ya ng’ombe tukajua huyu ni Aina flani na huyu ni aina flani
Happy Birthday,
Tunashukuru kwa kuendelea kufuatilia na kusoma majarida yetu. Tunashukur pia kwa ushauri wako
naitwa carle npo mwanza nmeanza ufugaji wa ng’ombe naomba ushauri kuhusu ufugaji
Habari,
Karibu sana. Unahitaji ushauri kuhusu nini hasa kwenye ufugaji wa ng’ombe