Vitungu saumu na vitunguu maji vina manufaa sana katika kukabiliana na aina mbalimbali za wadudu waharibifu na baadhi ya magonjwa. Harufu kali husaidia kuwafukuza wadudu kama vudukari, bungo na hata panya.
Saga kitunguu saumu kimoja, changanya kwenye lita moja ya maji na nyunyizia kwenye mazao. Unaweza pia kusaga vitunguu saumu 3, kisha changanya na mafuta taa, acha ikae kwa siku tatu, kisha ongeza lita 10 za maji ya sabuni na unyunyizie. Hii itaondoa aina nyingi sana ya wadudu wanaosababisha magonjwa.
Maoni kupitia Facebook