Heri ya mwaka mpya 2022
Ni matumaini yetu kuwa sote tumevuka salama na tumejiandaa vyema katika kuukabili tena mwaka huu kwa kishindo katika kilimo na ufugaji ili kuongeza tija na kukuza uchumi lakini pia tukizalisha kwa misingi ya kilimo hai kwa ajili ya kulinda afya zetu, wanyama, mazingira na mimea.
Ni hakika, mwaka uliopita haukuwa mbaya sana kwani pamoja na changamoto mbalimbali bado wengi wetu mmeturudia kwa shuhuda mkieleza ni kwa namna gani Mkulima Mbunifu imeweza kuwainua hatua moja mbele.
Tunawashukuru sana kwa namna ambavyo mmefanyika sehemu ya mradi huu kwa mawazo yenu lakini pia kwa kutekeleza yale ambayo yameelekezwa kupitia jarida letu pendwa la Mkulima Mbunifu.
Ni rai yetu basi, mwaka huu tuongeze bidii bale tulipolegalega, tutafute taarifa sahihi kabla ya kutekeleza jambo, lakini pia tushirikishe wataalamu wetu katika kutatua mambo mbalimbali yanayotukumba sisi kama wakulima na wafugaji wa kilimo hai.
Tunawatakia mwaka mpya wenye baraka na mafanikio tele.
KWAPAMOJA TUNAWEZA