- Kilimo

Kilimo hai kinachangia uzalishaji katika Kilimo

Sambaza chapisho hili

Tanzania ina ardhi yenye rutuba inayowezesha shughuli za kilimo hai kukua na kuongeza kipato kwa wakulima wadogowadogo. Hii inaweza kufanyika kwa kutumia teknolojia mpya inayoweza kusaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo mbayo yamezalishwa kwa kutumia kilimo hai, kwa ajili ya soko la ndani na la nje.

Njia tofauti za kilimo

Kwa kawaida viumbe hai wote ni wa asili. Fikra na mtizamo juu ya kilimo hai unaonekana kama vile viumbe hai wana sehemu yao maalumu ambayo ilikuwepo tangu miaka milioni nyingi iliyopita. Hii inajumuisha viumbe wadogo wadogo waliopo ardhini pamoja na kwenye mimea, wanyama na hata binadamu.

Kwa hakika kilimo kinategemea kwa asilimia kubwa uhalisia katika kuzalisha chakula. Ni muhimu basi kufanya utunzaji wa rasili mali zinazohitajika katika kilimo, na kuepuka teknolojia ambazo zinaweza kuwa hatarishi kwa afya za watu na mazingira.

Kilimo hai kinajaribu kuangalia na kupata picha nzima ya mazingira-si tu aina moja ya wadudu wanaweza kuuliwa, lakini kinajaribu kuweka sawa shughuli za kilimo kwa njia ya asili na uzalishaji wa chakula na mazao mengine kwa mzunguko wa kiasili.

Shirika la kimataifa la harakati na mwendelezo wa kilimo hai IFOAM, limeweka mikakati na mbinu za asili katika kilimo hai kwa kuangalia maeneo muhimu manne: Afya, ikolojia, usawa, na uangalifu.

Afya ya udongo, mimea, binadamu na wanyama

Kilimo ni lazima kiwezeshe na kuongeza afya ya udongo, mimea, wanyama na binadamu. Udongo ni nguzo muhimu katika maisha ya viumbe wote kwa ujumla. Udongo ulioharibiwa unaweza kuzalisha chakula kizuri, lakini kusiwe na malisho ya kutosha kwa ajili ya mifugo. Ili kuweza kupata chakula cha kutosha kwa ajili ya binadamu na malisho kwa wanyama, ni lazima kuboresha rutuba katika udongo. Afya ya binadamu na wanyama inaunganishwa moja kwa moja kwenye umuhimu na uwezo wa udongo kuzalisha.

Usawa katika mahusiano

Wakulima  wanaofanya kilimo hai wanahitaji kuona kuwa wanashirikishana maisha katika ulimwengu huu na viumbe hai wote, pamoja na hayo binadamu na wanyama wanatakiwa kupata nafasi yao ya kuwa na afya na furaha.

Tahadhari

Wakulima wa asili hutekeleza majukumu yao kama watumiaji makini wa ardhi. Ardhi ya kilimo na miundo mbinu mingine kama vile maji, ni lazima zitunzwe katika hali nzuri, kwa ajili ya kizazi kijacho. Watu na wanyama ni lazima watunzwe na kuangaliwa kwa umakini ili kuhakikisha afya zao zinaendelea kuwa salama. Teknolojia ya kisasa, pamoja na njia za kiasili ni lazima zinchunguzwe na kuangaliwa kwa kufuata taratibu hizi za kiasili. Tahadhari na kuzuia ni lazima zizingatiwe kuzuia hatari zinazoweza kujitokeza, na maamuzi ni lazima yazingatie thamani na mahitaji ya wote wanaoweza kuathiriwa.

Mbinu za kilimo hai kwa ufupi

Kilimo cha asili  

Mfumo wa kilimo cha asili unajumuisha muundo wa kilimo cha jadi ambao umekuwa ukitumika kwa karne nyingi sasa. Kwa kawaida hufanya matumizi mazuri ya miundo mbinu inayopatikana kwa njia za kienyeji, hili hali ikolojia na mahusiano hayabadiliki.

Kulima kwa kufuata desturi

Kulima kwa kufuata mila na desturi kulipindukia kufuata maendeleo ya kilimo katika karne iliyopita: Matumizi ya mashine katika kilimo, matumizi ya madawa, mbolea za viwandani, mbegu chotara, na kutumia kilimo cha umwagiliaji. Mabadiliko katika teknolojia ni lazima yalenge kukuza uzalishaji duniani kote.

Ongezeko la mabadiliko katika kilimo pia hujumuisha athari kama vile uchafuzi na uharibifu wa mazingira, uharibifu wa ardhi, au kuwa tegemezi kwa aina chache za mazao.

Kilimo hai

Kilimo hai kinajumuisha kujifunga kimaadili na kufanya maamuzi kuwa hautatumia  teknolojia ambayo itasababisha madhara kwa binadamu pamoja na mazingira.

Wakulima wanaofanya kilimo hai ni wachache sana duniani (lakini wanaongezeka). Kwenye nchi ambazo kilimo hai kimefanikiwa, na soko la mazao ya kilimo hai limeendelezwa, wanaweza kufikia resheni ya soko kwa asilimia 5-10, ingawa inaweza kutofautiana kulingana na ukanda.

Kilimo mseto

Mtindo wa kilimo mchanganyiko unajumuisha faida za mbinu zote zinazotumika katika kilimo. Kinajaribu kupunguza na kuepuka madhara yanayotokana na kilimo cha kisasa kwa kujumuisha mbinu za kilimo hai, kwa kupunguza matumizi ya mbolea za viwandani na kemikali, na kuchagua kwa uangalifu viuatilifu. Katika nchi nyingi hii inaonekana kuwa njia sahihi ya kurekebisha madhara yanayotokana na kilimo cha kisasa.

Virutubisho hai

Mbole zisizo za asili hazitumiki katika kilimo hai. Virutubisho vya asili vinavyotokana na mimea hutumika kurutubisha udongo,si mimea. Kuongeza rutuba kwenye udongo huchukuliwa kama nguzo muhimu. Mbolea za asili hutumika kuboresha au kushikilia rutuba ya udongo, hii inaweza kufanyika kwa kuongeza mbolea inayotokana na mifugo, mbolea vunde, na kuacha mabaki ya mazao shambani yatumike kama matandazo. Mbolea za asili huwa na virutubisho kama vile Nitrojeni, Fosifeti, na Potashiamu. Virutubisho hivi hupatikana kwa ajili ya mimea wakati viumbe hai wadogo walioko kwenye ardhi wanapovunja vunja mbolea hizo wakati wakila.

  • Nitrojeni (N): Chanzo kizuri cha asili cha Nitrojeni kwa mimea kinatokana na mkojo wa wanyama na aina zote za kinyesi cha wanyama, hasa kinachotokana na nguruwe na kuku. Mbolea inayotokana na mimea na wanyama hutoa nitrojeni nzuri kwa mimea. Mimea jamii ya mikunde na mbolea vunde ni chanzo kizuri cha asili kuweza kupatia mimea nitrojeni.
  • Fosiforasi (P): Njia za asili za kupata fosiforasi ni kupitia mbolea ya miamba, mbolea ya kuku, na wanyama wengineo.
  • Potashiamu (K): Njia za asili za kupata potashiamu ni majivu, kinyesi cha mbuzi na kondoo, kuku, na mifugo mingine.

Ni faida gani zinazoweza kutarajiwa kutokana na kilimo hai?

  • Kilimo hai huongeza rutuba kwenye udongo kwa muda mrefu. Udongo hai una kiasi kikubwa cha vitubisho vinavyotokana na uozo wa malighafi za asili. Pia huongeza uwezo wa ardhi kuzalisha, kuhifadhi maji kwa muda mrefu na kukabiliana na ukame.
  • Kilimo hai hakihitaji kuwekeza gharama kubwa. Kilimo hai hutumia miundo mbinu inayopatikana hivyo kumuepushia mkulima mdogo gharama za madawa ya viwandani.
  • Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa kilimo hai kinaweza kuchukua nafasi ya aina nyingine za kilimo katika nchi zinazoendelea: Kilimo hai kinaongeza mavuno kwa mkulima baada ya muda mrefu, wakati amewekeza kidogo, na wakati huo huo kiasi kikubwa cha mazao kikizalishwa. Hii humfaidisha mkulima mdogo, ambae mara nyingi yuko kwenye hatari ya kukumbwa na upungufu wa chakula, utapia mlo na madeni.
  • Kilimo hai hakimuweki mkulima pamoja na familia yake katika athari ya kupata magonjwa yanayotokana na matumizi ya kemikali na mbolea za viwandani.
  • Kilimo hai kinajumuisha tafiti za kisayansi na kilimo cha kijadi katika kilimo endelevu.
  • Hata kama kanuni za kilimo hai hazijazingatiwa ipasavyo, na hata kama hakuna soko la mazao ya kilimo hai yaliyozalishwa, mazao na bidhaa zake yanaweza kupatikana, na shamba pia kufaidika kwa kutumia mbinu za kilimo hai.
  • Kilimo hai huifadhi mazingira, afya ya binadamu, na wanyama.

 

 

 

 

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

4 maoni juu ya “Kilimo hai kinachangia uzalishaji katika Kilimo

      1. Habari, Karibu sana Mkulima Mbunifu
        Ni kweli bila kufuata kanuni za msingi kabla ya kuzalisha zao lolote hakika ni lazima utazalisha kwa hasara, hivyo ni muhimu kufahamu muda sahihi wa kulima zao husika, pakununulia mbegu bora na pembejeo mbalimbali, kugahamu kuhusu shamba na udongo wa eneo lako kisha kulirutubisha, kufahamu soko liko wapi na kuwa karibu na maafisa ugani ili waweze kukushauri pale inapotakiwa.

    1. Habari, Karibu sana Mkulima Mbunifu
      Ni kweli kilimo hai kina faida kubwa sana kwenye udongo, na urutubishaji wa udongo hupelekea uzalishaji bora wa mazao na baadaye soko bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *