- Binadamu, Kilimo, Mimea

Fahamu aina mbalimbali za viungo muhimu kwa afya ya binadamu

Sambaza chapisho hili

Pamoja na viungo kutumika kuongeza ladha katika vyakula, pia vina manufaa katika mwili wa binadamu.

Mara nyingi wakulima wamekuwa mstari wa mbele kuzalisha mazao muhimu kwa manufaa ya jamii, ilhali wao wakijisahau kuwa wanahitaji pia kutumia ili kuimarisha afya zao.

Viungo mbalimbali kama tangawizi, vitunguu saumu, vitunguu maji, pilipili na limao ni muhimu katika kuimarisha kinga ya mwili.

Je ni virutubisho gani vinavyopatikana katika viungo hivyo!

Kitunguu swaumu (Allium sativum): Hii ni aina ya tunguu ambalo hutumika kama kiungo katika chakula. Vilevile huaminika kutibu maradhi mbalimbali katika mwili wa binadamu.

Kitunguu maji:  Ni kiungo ambacho kina virutubisho katika vyakula, kina salfa ambayo ni nzuri, hasa kwenye ini na inasadikika kuwa husaidia kuponya maradhi mbalimbali kwenye utumbo na kinywa kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya vitamini C.

Tangawizi: hutumika kama kiungo katika vyakula mbalimbali, pia dawa kwa tiba ya magonjwa ya binadamu na wanyama na kiambato muhimu kwenye vinywaji mbalimbali. Tangawizi pia imegundulika kupunguza kwa kiasi kikubwa lehemu katika mishipa ya damu na kuzuia damu kuganda katika mishipa hiyo, hivyo kuzuia kutokea madhara ya kuziba kwa mishipa ya damu.

Pilipili kichaa Ina wingi wa vitamini A, pia ina vitamini B, vitamini E, vitamini C, Riboflavin, Potassium na Manganese. Ni dawa yenye nguvu sana na matumizi mengi, hutumika kwa kusafisha damu na kutoa sumu mwilini,pia hutumika kusisimua mzunguko wa damu na kuweka sawa uwiano wa
tindikali(acid)mwilini.

Limao (Citrus limon): Hili ni tunda la mlimau, na ni mti mdogo ambao daima huwa ya  kijani kibichi na huaminika kama msaada mkubwa wa umengenywaji wa chakula. Limau ina vitamini C nyingi ndani yake na kiasi kidogo kinatosheleza mahitaji ya binadamu.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *