Mbegu ni nini?
Mbegu ni sehemu ya mmea ambayo ina uwezo wa kuota na kutoa mmea mpya.
Kuna makundi makuu mawili ya mbegu tunayoyazungumzia katika kilimo ambayo ni punje na shina/ mizizi.

Punje
Hizi ni mbegu za nafaka au za matunda, ambazo huzalishwa kwa uchavushaji. Kawaida huwa na kiini na chakula chake huhifadhiwa ndani ya ganda gumu la mbegu. Mfano, mahindi, maharage, mtama.
Shina/mizizi
Hizi ni sehemu za mimea kama vile mihogo, viazi vitamu, au viazi mviringo, ambazo hutumika kama mbegu kwa ajili ya upandaji na kuzalisha mimea mipya.
Maoni kupitia Facebook




