- Kilimo

Kuhusu kuandaa mashimo ya migomba na aina za migomba katika shamba moja

Sambaza chapisho hili

Musa Hamisi anauliza: Za majukumu Mkulima Mbunifu, naomba kujua ni kipindi gani napaswa kuandaa mashimo na Je, naweza kupanda migomba aina 3 tofauti ndani ya shamba moja lenye ekari moja?

Mkulima Mbunifu: Habari, Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma machapisho ya MkM. Migomba huhitaji Kiasi cha chini cha mvua kifaacho ni 100mm kwa mwezi au 1200mm kwa mwaka.

Mwinuko ni kutoka usawa wa bahari hadi mita 1800 juu ya usawa wa bahari. Zaidi ya mwinuko huo migomba haikui vizuri. Kiasi cha joto kinachofaa ni nyuzi joto za sentigredi 25 hadi 30 chini ya nyuzi joto 16 migomba haikui vizuri.

Migomba hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha, kina kirefu, usiotuamisha maji na pia usiwe na chumvi. Kwa maana hiyo hakikisha hali ya hewa hii ndiyo iliyo katika eneo lako na ni vyema kupanda msimu wa mvua au kama hakuna mvua uwe na umwagiliaji.

Uchimbaji wa mashimo unafaa ufanywe mapema kiasi cha juma moja hadi mwezi kabla ya muda wa kupanda. Pia unaweza kuotesha aina mbalimbali za migomba katika shamba moja lakini ni vyema upande katika mistari kila aina ya mgomba/ndizi.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *