Mohd Rafii anauliza: Waungwana nisaidieni, Matumizi ya mwarobaini kwa kuulia wadudu katika mimea niuchemshe au niusage tu na kuuloweka?
Mwarobaini ni mti unaostahimili ukame, unatoa kivuli na pia umeonekana kuwa na manufaa
makubwa kama tiba kwa binadamu na mafuta yake hutengeneza sabuni.
• Kati ya dawa zote za asili, mwarobaini umeth ibitika kufanya vizuri zaidi kutokana na uwezo
wake maradufu
• Mwarobaini unaonyesha matokeo mazuri kuliko baadhi ya dawa za viwandani
Matumizi ya Mwarobaini
Kutengeneza dawa kutokana na mbegu
• Twanga mbegu kiasi zilizokomaa na kukaushwa ili kupata unga
• Changanya na maji lita 1.
• Nyunyizia bustani kuzuia wadudu.
Au
• Lainisha mbegu gramu 500 kisha twanga
• Ongeza maji lita 10 kisha iache ikae usiku mmoja
• Chuja kwa kitambaa kisha nyunyizia kwenye mimea
• Rudia kila baada ya siku 10-15 au kila wiki endapo kuna wadudu wengi.
Au
• Saga kilo 2 za mbegu
• Changanya na maji lita moja
• Acha kwa usiku mmoja
• Ongeza maji lita 10
• Nyunyizia mimea