Madhumuni ya kipindi hiki ni kukuelimisha kuhusu Kilimo Endelevu na mfumo wa uzalishaji unaohakikisha uendelevu katika kilimo, na kuongeza kipato hasa kwa wakulima wadogo ambao ni idadi kubwa humu nchini. Hii ikiwa ni pamoja na Kilimo hai.
Mkulima Mbunifu ni jarida la kila mwezi linaloangazia mbinu na teknologia za kilimo endelevu cha kiikolojia, uzalishaji wa kilimo hai na kuboresha maisha ya kiuchumi, kijamii na mazingira kwa wakulima wadogo.
Mkulima Mbunifu inafanya mambo mengi, lakini kubwa na muhimu ni huduma ya kusambaza habari na elimu kuhusu mbinu bora za kilimo ili kuongeza pato kupitia shamba hasa kwa wakulima wadogo kupitia vikundi vyao, maafisa ugani, na mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za kiserikali.
Lengo kubwa ni kumuona mkulima mwenye furaha, anayefanya vizuri kazi ya kilimo na kupata mapato ya kutosha kutimiza majukumu ya kila siku.
Tunakuletea kipindi hiki cha redio ili kujenga uelewa juu ya upatikanaji wa jarida la MkM, faida zake na jinsi wakulima wanavyoweza kulipata, na kuwafikia wakulima wengi zaidi.
Sikiliza Makala ya Kwanza