- Kilimo, Mimea

Samadi ya wanyama na mimea

Sambaza chapisho hili

Ubora wa samadi ya wanyama hutegemea zaidi kile kilicholiwa na mnyama. Ikiwa wamelishwa chakula duni au nyasi zilizomea katika udongo usio na rutuba, basi samadi yao pia itakuwa na ubora duni.

Ikiwa wanyama wamelishwa chakula kizuri basi samadi pia itakuwa bora na iliyojaa virutubisho.

Samadi iliyo tayari kwa matumizi

Samadi huhitaji kupevuka kwa majuma au miezi kadhaa kabla ya kuwa tayari kutumiwa mashambani kama mbolea. Hata hivyo kiwango cha naitrojeni kilichomo katika samadi hiyo hupungua muda unavyopita kwa kupotelea hewani au kufagiliwa mbali na maji ya mvua.

Ili kuzuia hili kutokea, unashauriwa kuiweka samadi katika shimo, au pipa lilofunikwa kabla ya kupeleka na kuitandaza shambani.

Samadi iliyochanganywa na mkojo kwa mfano ikiwekwa katika shimo ambamo kuna tope laini huwa na kiasi kikubwa cha naitrojeni kuliko samadi yenyewe.

Hata hivyo, naitrojeni iliyo katika mkojo hupotea kwa urahisi hivyo funika shimo hilo la tope ili kuzuia upotevu huu. Hata kama samadi ipo katika hali duni, bado inakuwa mbolea nzuri hivyo unapaswa kuitumia.

Kwa ujumla, samadi ya nguruwe na kuku huwa bora zaidi kuliko ya ng’ombe na mbuzi lakini unaweza kuistawisha samadi ya ng’ombe wa kuichanganya na samadi ya wanyama wengine.

Mwonekano wa mbolea ya samadi iliyotayari kutumika shambani

Namna ya kutumia samadi ya mimea na wanyama

Wakulima huweza kuchagua njia ya matumizi ya mabaki ya mazao mbalimbali kwa kufanya yafuatayo;

  • Kuchagua mabaki kutoka katika aina tofauti ya mimea kama vile miti na masalia ya mazao.
  • Kuchagua mabaki ya mimea kutoka sehemu mbalimbali ndani ya shamba au nje ya shamba.
  • Kutumia mabaki moja kwa moja shambani au kuyarundika na kuzalisha mbolea kisha kutumia.
  • Kuchanganya mabaki ya mimea ya aina mbalimbali kwa pamoja.
  • Kuweka mabaki ya mimea juu ya udongo kama matandazo au kuchanganya na udongo wakati wa kulima shamba.
  • Kuweka mabaki juu ya shamba na kuacha kabla ya kulima.
  • Kutumia mabaki kutilia mbolea mazao yanayohitaji virutubishi kwa wingi kama vile mboga au mazao makuu kama mahindi.
  • Mara baada ya kufahamu ubora wa mabaki unayohitaji kutumia ni lazima sasa uamue jinsi ya kuyatumia kutegemeana na aina ya mabaki kama miti au samadi.
  • Unaweza kuchanganya mabaki yayo katika udongo na ukatumia kama mboji au ukaweka juu ya udongo kama matandazo.
  • Ni vizuri kutumia mabaki yaliyobora moja kwa moja kama mbolea katika udongo na kwa aina nyingine ya mabaki kama mabua ya mahindi ni bora yatengenezwe mboji kwanza au yachanganywe na mbolea kabla ya kuwekwa shambani.
  • Aina nyingine ya mabaki kama vile mashina na matawi hayawezi kuwa mboji kwasababu ina uwingi wa mitimiti hivyo ni muhimu kutumika kama kizinga mmomonyoko wa udongo ka kusaidia kuhifadhi unyevu wa ardhi.
  • Ikiwa kuna mabaki yenye ubora na yaliyo duni, ni vyema kuchanganya kabla ya kuweka shambani. Changanya mabaki ya mimea na mabaki ya wanyama ili kuweza kustawisha samadi ya hali duni.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *