Katika majarida yaliyopita, tuliangazia kwa undani kuhusu sumu kuvu na namna ya kudhibiti. Katika toleo hili tumeona vyema kurudia makala hii hasa kwa kuwa tunaelekea msimu wa mavuno na wakulima wanahitaji kukinga mazao yao na sumu kuvu.
Sumu kuvu (Aflatoxin) ni aina za kemikali za sumu zinazozalishwa na aina ya ukungu au fangasi wanaoota kwenye mbegu za nafaka kama vile mahindi, mbegu za mafuta kama karanga, jamii ya kunde, mazao ya mizizi na pia vyakula na malisho ya wanyama.
Katika mazao yaliyovunwa, sumu kuvu inayotengenezwa na ukungu huingia katika nafaka iliyohifadhiwa katika sehemu ambayo kitaalamu haijakidhi vigezo vya kuhifadhia nafaka.
Upo uwezekano mkubwa kwa baadhi ya nafaka kuanza kuoza na kutengeneza ukungu huu ambao unaambatana na sumu kuvu ndani yake ikiwa nafaka hiyo haijavunwa shambani mapema baada ya kukauka na baadaye mvua au unyevu mkubwa ukaingia shambani.
Fuatana nasi katika toleo lijalo la Mkulima Mbunifu ili kujua namna ya kudhibiti sumu kuvu katika mazao yako.
Maoni kupitia Facebook