Utunzaji bora wa majike ni muhimu kwani utamuwezesha mfugaji kupata mazao mengi na bora. Majike wazazi watunzwe vizuri ili kuongeza idadi ya watoto watakaozaliwa kwa mwaka na kuongeza faida kwa mfugaji.
Utunzaji bora ni kiini cha idadi ya watoto watakaozaliwa,watakaoishi na Muda wataochukua kufikia uzito kuuza na gharama zitakazotumika.
Kuchagua jike bora
Mfugaji anashauriwa kuchagua nguruwe jike anayetegemewa kuwa mzazi kwa kuzingatia sifa zifuatazo:-
- Awe amezaliwa na mama anayezaa watot wengi,menye kutoa maziwa mengi na mtunzaji mzuri wa Watoto.
- Awe na afya nzuri
- Awe na kiwele kikubwa chenye chuchu kati ya 10 hadi 14
- Awe ni MRE na mwenye uwiano mzuri kati ya urefu, upana na kimo
- Awe na umbile la kumuwezesha kubeba mimba na kuzaa kwa urahisi
- Awe na miguu imara iliyonyooka,kwato imara,mgongo wenye nguvu na uliopinda kiasi
- Awe mpole
- Atokane na wazazi wasiokuwa na historia ya magonjwa au klema cha kurithi.
Taratibu za kupandisha majike
Nguruwe jike anaanza kuonyesha dalili za joto akiwana umri wa miezi sitahadi saba.Hata hivyo, inasshauriwa kutompandisha kipindi hicho ili kuzuia kuzaliwa watoto wenye uzito mdogo,kupata mtatizo wakati wa kuzaa,afya mbaya na kudumaa. Hata hivyo, inapendekezwa nguruwe apandishwe atakapoonyesha dalili za joto kwa mara ya pili au ya tatu.
Kwa kawaida nguruwe huwa tayari kupandishwaakiwa na umri wa miezi kati ya nane na tisa kutegemea afya na aina ya nguruwe.
Kumtambua Nguruwe Aliye Kwenye Joto
Mfugaji anashauriwa kuwachunguza nguruwe siochini ya mara mbili kwa siku hususani asubuhi na jioni wakati wa kuwalisha ili kutambua dalili za joto.
Zifuatazo ni daliliza nguruwe jike aliye kwenye joto
- Hupoteza hamu ya kula
- Hutoa sauti ya kugugumia
- Huhangaika mara kwa mara
- Hupandwa na wenzake na hutulia akipandwa au akigandamizwa mgongoni
- Sehemu ya uke huvimba na huwa nyekundu
- Hukojoa mara kwa mara na hutoa ute
- Husimama wima na hutulia akiwa ametanua miguu ya nyuma na mkia ukielekea juu wakati akipandwa na dume.
Dalili hizi sio lazima zionekane zote wakati mmoja hivyo ni jambo la muhimu kuwa mwangalifu.Ili dalili hizi ziweze kuonekana vizuri,chumba cha majike yanayotarajiwa kupandwakinatakiwa kiwe karibu na cha dume.
Joto hudumu kwamuda wa sikumbili hadi tatu.Nguruwe jike apandishwe mara mbili kwa siku hususani asubuhi na jioni. Nguruwe apandishwe masaa 12 hadi 24 anapoonyesha dalili za kusimama akipandwa na dume au akigandamizwa mgongoni.
Kwa kawaida nguruwe hurudia kuingia kwenye joto kila baada ya siku 21 ikiwa hana mimba.Mfugaji anashsuriwa kumchunguza ngurwe jike baada ya kumpandisha aingia kwenye joto baada ya kupandishwa.
Wakati wa kupandisha inashauriwa nguruwe jike kupelekwa kwenye chumba cha dume ili kuzuia dume kushambuliwa na jike.Nguruwe ambaye hashiki mimba baada ya kupandishwamara nyingi inashauriwa mfugaji kumuona Daktari wa mifugo kwa ushauri.
Ulishaji wa jike
Kabla ya kupandishwa nguruwe jike apewe kilo 2.5 hadi 3 za chakula kwa siku na kupewa maji safi na ya kutosha wakati wote.
Kutunza Nguruwe Wenye Mimba
Utunzaji bora wa nguruwe wenye mimba ni muhimu katika kupata watoto wenye uzito mkubwa na afya bora.Pia husaidia nguruwe kuwa na afya bora,kutoa maziwa mengi nakupunguza vifo vya watoto.
Mimba ya nguruwe huchukua siku 114hadi 119(miezi mitatu,wiki tatu na siku tatu) hadi kuzaa.Kwa kipindi hicho nguruwe anahitaj lishe bora na maji,hewa safi nay a kutosha, mazoezi pamoja na kinga dhidi ya magonjwa.Hivyo, inashauriwa banda liwe na nafasi ya kutosha, na safi muda wote.
Ulishaji wa Nguruwe Wenye Mimba
Nguruwe mwenye mimba anahitaji kupewa cha kula kinacholeta nguvu na kujenga mwili. Inashauriwa, mwezi wa kwanza wa umri wa mimba apewe kilo 2 hadi 2.5 kwa nguruwe mwenye afya nzuri, akiwa dhaifu apewe kilo 3 kwa majuma matatu.
Pia, baada ya siku 84 za umri wa mimba apewe kilo 2 za chakula kwa siku na kuongeza nusu klo kila wiki mpaka siku ya tatu kabla ya kuzaa. Siku tatu kabla ya kuzaa, chakula kipunguzwe hadi kufikia kilo 2 kwa siku na wapewe majani kama luseni au chakula chenye nyuzi nyuzi nyingi kama pumba kilo moja kwa siku tatu kabla ya kuzaa ili kuzuia tatizo la kinyesi kuwa kigumu ambacho hushindwa kutoka na kusababisha nguruwe kuzaa kwa shida. Siku ya kuzaa nguruwe asipewe chakula apewe maji tuu.
Kinga dhidi ya Maginjwa na Wadudu
Nguruwe wenye mimba huathiriwa zaidi na minyoo na magonjwa mengine. Minyoo hupunguza hamu ya kula na hivyo huathiri afya ya nguruwe pamoja na ukuaji wa mimba. Uzuiaji wa magonjwa na wadudu ni muhumu kwa afya ya nguruwe mwenye mimba. Mfugaji anashauriwa kuwapa nguruwe dawa ya kuzuia minyoo siku 21 hadi 28 kabla ya kuzaa.
Kuzuia wadudu, mfugaji anashauriwa kuogesha kwa dawa zakuogeshea angalau mara mbili kwa wiki ili kuzuia ukurutu na matatizo mengine ya ngozi. kwenye sehemu ambazo kuna ndorobo, mfugaji anashauriwa kuwachanja nguruwe. Ni muhimu banda na vifaa vya kulishia na maji viwe safi wakati wote.