- Kilimo

Tumia Azola kama mbolea katika kilimo hai

Sambaza chapisho hili

Azola ni majani au magugu ambayo huota sehemu yenye maji kwa wingi. Mmea huu umekua ukitumiwa zaidi na wafugaji wengi kama chakula mbadala kwa kuku. Huweza kuliwa na kuku ikiwa mbichi au fresh au ukivunwa na kuanikwa kisha kuchanganywa kwenye chakula cha kuku.

Majani haya huweza kutumika kulisha mifugo mingine kama vile bata, ng’ombe, nguruwe, mbuzi, kondoo, sungura na pia ni chakula kizuri sana kwa samaki wanaofugwa kwenye mabwawa kama vile kambale (african catfish), sato (tilapia).

Majani haya yanasifika kwa kuwa na virutubisho vingi protini, vitamins A & B12, amino asidi pamoja na madini mbalimbali ya kalsiamu, potasiamu, magnesiamu, fosiforas.

Unawezaje kutumia Azola kama mbolea

  • Azola inaweza kutumika kama mbolea kwa kuotesha shambani moja kwa moja kwenye shamba lililooteshwa mazao kama vile mpunga ambapo maji yanatuama.
  • Azola husambazwa shambani moja kwa moja mara baada ya kuvuna kisha kuvuruga/kuchanganya na udongo wakati wa kulima kama tunavyofanya samadi.
  • Vuna Azola kisha ianike kwenye kivuli ikishakauka isage ili kupata unga kisha weka kwenye mashina ya mimea yako au kama nyingi mwaga kwenye mtaro shambani ijichanganye na udongo.
  • Mara baada ya kuvuna iache ioze kisha changanya na mbolea kama samadi au ya kuku na weka kwenye kiroba kisha dumbukiza kwenye maji ijichuje upate ikiwa kimiminika. Kama ikiwa nzito changanya na maji kiasi kisha tumia njia ya matone kuweka kwenye mimea yako au tumia bomba kunyunyuzia kwenye mimea.
  • Vuna azola ikiwa mbichi kisha weka majani yake chini ya shina la kila mmea.
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *