- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Kutuhusu, Masoko, Mazingira, Mifugo

Shiriki kongamano la pili la kiikolojia Afrika Mashariki (EAAC2025)

Sambaza chapisho hili
Shirika la Biovision Africa Trust (BvAT) ambalo ni mshirika wa MkM linaanda kongamao la kujadili maswala ya ikolojia na wakulima Afrika Mashariki. Hii ni fursa nzuri ya wakulima na wadau wa kilimo ikolojia kushirikishana njia na mbinu za kupanua na kusambaza uelewa na habari za mbinu endelevu za uzalishaji.
Kongamano hili litafanyika Nairobi, Kenya, tarehe 25-28 mwezi wa Machi mwaka huu (2025) katika hoteli ya Argyle Grand.  Baadhi ya maswala yatakayoangaziwa ni usalama wa chakula, lishe na afya, rutuba ya udongo na mifumo ya mbegu inayosimamiwa na wakulima, sera muwafaka zinazosaidia wakulima kutumia mbinu endelevu, uwekezaji na fedha za kuinua kilimo na uwezo wa wakulima kuzalisha zaidi.
Unaweza kujisajili kushiriki kwa kutembelea tovuti https://ea-agroecologyconference.org au wasiliana na MkM kwa habari zaidi. Itakuwa vyema watanzania kushiriki na kuchangia mwelekeo wa kilimo ikolojia Afrika Mashariki. Kuna mambo mengi mazuri ambayo wakulima wetu wanafanya, na hii ni fursa muhimu ya kushirikishana uzoefu na mbinu zinazofanya kazi, hasa yale yanayopunguza gharama za uzalishaji, kupanua mapato na kuzalisha chakula safi na salama kwa kaya, jamii, nchi na eneo zima la Afrika Mashariki.
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *