Hili ni swali alilouliza mkulima Nelson Shao.
Habari Nelson , Karibu sana Mkulima Mbunifu na hongera kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za Mkulima Mbunifu. Kuhusu chakula cha kuku unaweza kutengeneza mwenye kama ifuatavyo;
Malighafi aina ya kwanza na kiwango
- Mahindi kilogramu 40
- Pumba ya mahindi kilogramu 25,
- Mtama kilogramu 5
- Mashudu ya alizeti kilogramu 10
- Dagaa kilogramu 4
- Damu kilogramu 5
- Mifupa iliyosagwa kilogramu 4.50
- Chokaa kilogramu 4
- Vitamini kilogramu 2
- Chumvi kilogramu 0.50
Mchanganyiko huu wote utaleta jumla ya kilogramu 100 za chakula.
Hivyo utakapolisha kuku, watakuwa wamepata viini vyote kwa uwiano sawia unaotakiwa mwilini.
Malighafi aina ya pili na kiwango
Aidha, unaweza pia kujumlisha mchanganyiko huu na ukawa na uwiano sawa wa virutubisho kama ulivyo mchanganyiko wa kwanza.
- Dagaa kilogramu 4.5
- Soya kilogramu 18
- Mahindi kilogramu 50
- Pumba ya mahindi kilogramu 15
- Mashudu ya pamba kilogramu 5
- Mifupa iliyosagwa kilogramu 3
- Vitamini kilogramu 2
- Chumvi nusu kilogramu (0.5)
- Chokaa kilogramu 2.
Yote jumla kilogramu 100.
Mara utakapotengeneza chakula hiki, hakikisha unakihifadhi sehemu salama, kavu na yenye hewa safi. Ni vyema kutengeneza chakula kwa kiwango kidogo ili kisikae sana muda mrefu bila kutumiwa kuepusha uharibifu.
Unaweza kutengeneza chakula cha kilogramu 50 badala ya 100, kwa mchanganyiko huo huo, isipokuwa kiwango katika kila malighafi utagawa nusu yake.
Maoni kupitia Facebook