- Kuku, Mifugo

MATUNZO SAHIHI YA VIFARANGA VYA KUKU

Sambaza chapisho hili

Ni muhimu mfugaji kufahamu kuwa kifaranga wa leo ndiye kuku wa kesho atakaesababisha mafanikio yake na kufanya maisha yasonge mbele bila kikwazo.

Ufugaji wa kuku ni moja ya shughuli ambayo imejipatia umaarufu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa wakulima na hata wanaofanya shughuli nyinginezo tofauti na ufugaji peke yake.

Ili kuwa na mafanikio ya uhakika ni muhimu kwa mfugaji kuzingatia taratibu zote za ufugaji wa kuku akianzia kwenye utunzaji wa vifaranga ambao ndio kuku wa baadae.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ambayo mfugaji anapaswa kufuata na kuzingatia:

Chakula: Hakikisha vifaranga wanapewa chakula sahihi na kiasi kile kinachopendekezwa kwa umri na uzito hai husika

Mfano: Wape chick mash vifaranga wa siku moja hadi wanapofikia umri wa mwezi mmoja baada ya hapo watapewa chakula kinachoitwa grower’s marsh/finisher’s mash. Usikae zaidi ya masaa mawili (2) bila ya kuwapa chakula kingine.

Usafi:

Vyombo vya chakula na               maji.

  • Hakikisha chakula safi na maji safi vinapatikana wakati wote. Madini, vitamini na viuatilifu vinawekwa kadri inavyoshauriwa na wataalamu wa mifugo.
  • Fanya usafi wa kutosha na kuweka dawa kabla ya kuhamishia kuku bandani.
  • Mazingira ya ndani na nje ya banda ni lazima yawe safi na makavu daima kwani uchafu na unyevunyevu ni chanzo cha vijidudu vya magonjwa kama vile minyoo na kuhara damu.
  • Epuka usumbufu (stress) mahali wanapoishi vifaranga.

Mfano: a) Epuka Kuondoa mfuniko (hoover) wa brooder kila mara.

  1. b) Epuka pia kubamiza milango kwa nguvu.
  2. c) Usiruhusu wageni kuingia kwenye banda bila mpangilio.
  3. d) Epuka kukaa muda mrefu bila kuwapa chakula.
  4. e) Kuwepo kwa joto jingi katika chanzo.
  5. f) Utaratibu usiwe wa kubadilika badilika mara kwa mara mfano chakula na maji.
  6. g) Chunguza vifaranga kabla ya kwenda kulala na baada ya kuamka. Utaratibu unaokubalika ni kukesha kwa zamu ili vifaranga wasije wakalaliana na hivyo kusababisha vifo vyao. Kazi ya kulea vifaranga ni ya kujitolea sana hasa katika wiki tano za mwanzo.

Mabanda             yawe     safi na makavu wakati wote ili kuzuia mazalia na chanzo cha maambukizi kutokana na unyevunyevu. Mwanga na mzunguko wa hewa ya kutosha:

Kuna vyanzo viwili vya mwanga ambavyo ni

  1. Taa ya kandili (kerosene lamp)
  2. Taa inayotumia nguvu za umeme (balbu) kama vile (infrared bulbs).

Mwanga na mzunguko wa hewa ndani ya bruda ni muhimu kwani huvutia na kuvishawishi vifaranga kuanza kula. Weka madirisha makubwa yenye kuingiza hewa safi na kutoa ile chafu. Banda lisilo na hewa ya kutosha huchochea kuenea kwa magonjwa ya mfumo wa hewa. Andaa nafasi ya kutosha ili kuepuka vifaranga au kuku kurundikana.

 Chakula bora na cha kutosha

  1. a) Wape vifaranga chakula cha kutosha, kizuri na chenye viini lishe vyote.
  2. b) Wape chakula vifaranga kwa vipindi vilivyopangwa badala ya kuwapa mfululizo ili wapate muda wa kutumia chakula walichokula vizuri mwilini.
  3. c) Hakikisha vyombo vya chakula havikai bila chakula.

Madawa:

  • Dawa inatakiwa             kuwekwa             ndani     ya           chakula na maji ili kuzuia ugonjwa wa kuharisha damu (coccidiosis).
  • Dawa ya           kideri     ni            vizuri     ikatolewa             wakati vifaranga wamefika na au siku chache baada ya kuingizwa kwenye brooder.
  • Vitamini huandaliwa         wakati   mwingine pamoja na madawa kama antibiotics ili zichanganywe kwenye chakula chao.
  • Zingatia ratiba ya           chanjo  inayopendekezwa na wataalamu.
  • Kuku wapewe               dawa     ya           kuzuia   maumivu ya usumbufu  kwa siku 2-5.

Vifaa ndani ya banda la vifaranga:

Vyombo vya chakula: Vyombo vya chakula  vitawekwa sehemu ifaayo na inayofikika na vifaranga. Hakikisha vifaa havichafuliwi na kinyesi cha vifaranga au takataka zilizomo ndani ya banda. Hakikisha unaongeza vyombo vya chakula na maji kadri vifaranga wanavyozidi kukua na kuongezeka uzito.

Vyombo vya maji: Ili kazi ya usafi iwe rahisi umbile na ukubwa wa vyombo vya maji viwe nusu mduara mfano wa mwanzi uliopasuliwa katikati. Mwanzi huu huwekwa katikati ya vijiti viwili vitakavyoushikilia. Vijiti hivi viwekwe katika namna ambayo ni rahisi kuvirekebisha. Vilevile kifaa hiki cha maji kinaweza kuwekwa kizibo ambacho kitalegezwa au kuondolewa wakati wa kusafisha. Inashauriwa kuwa vifaa vya kunyweshea viwe na ujazo wa lita tano. Vilevile vifaa hivi viwe vya plastiki ili kuepuka kuotesha kutu.

Ndoana: Hizi ni fimbo za miti au waya ambazo hutumika wakati wa kukamatia kuku kwa ajili ya tiba au kuwauza.

Toroli au mikokoteni: Ikiwa banda limejengwa vizuri, toroli linaweza kusadia kupunguza idadi ya masaa yatakayotumika wakati wa kulisha au kuweka maji.

Kuchagua kundi la vifaranga wenye afya njema:

Chagua  vifaranga wenye afya njema ambao hutambuliwa kwa kuwa na manyoya makavu, macho maangavu na walio wachangamfu. Chunguza vifaranga wenye kinyeo kilichochafuka na wazubavu na kisha uwatibu. Vifaranga dhaifu, wenye vilema na wagonjwa waondolewe katika kundi la kuku (culling).

Vifaranga wa mayai wahamishiwe kwenye banda la kukuzia wakiwa na umri wa wiki 6-8 ambako watakaa hadi wiki ya 16-18 kabla ya kuhamishiwa banda la kutagia.

Mabadiliko ya hali ya hewa: Wakati wa majira ya joto kuku hupunguza kula, hivyo wakati huu inashauriwa kumwaga maji

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

2 thoughts on “MATUNZO SAHIHI YA VIFARANGA VYA KUKU

  1. shukrani sana kwa elimu na ushauri. pia naomba utuwekee mfano wa dawa unapozungumzia dawa au vitamini maana wengine mazingira tuliyomo hatahao wataalamu hawapo tunategemea mitandao kama hivi.

    1. Habari, pole sana kwa changamoto. Dawa nyingi hatushauri mfugaji kutoa kwa wanyama au ndege ikiwa hajui namna sahihi ya kutoa hivyo tunashauri kuhakikisha unapata wataalamu wa mifugo au unapoenda kununua dawa za mifugo nunu mahali ambapo unajua utapata taarifa sahihi

Leave a Reply to Mkulima Mbunifu Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *