Katika kilimo, matumizi ya Molases ni muhimu kwa kuboresha hali ya udongo, kdhibiti wadudu, kuwezesha udongo kuwa na rutuba, kurekebisha hali ya udongo na pia kupunguza matatoizo kwa mimea inayopandikizwa.
Matumizi ya Molases husaidia kusafisha mipira ya umwagiliaji. Utafiti unaonyesha kuwa Molases husaidia kuboresha ubora wa udongo.
Matumizi na kiasi cha kutumia
- Kuboresha umbile la udongo molases husaidia kuboresha udongo na kuunganisha chembe za udongo na chembe za rutuba na viumbe hai ardhini. Ili kuwa namatokeo mazuri, Molasese ichanganywe kwenye udongo mfululizo kwa kiasi cha lita 20-25 kwa hekta kwa wiki na kipindi chote cha kumwagilia.
- Kuongeza viumbe hai kwenye udongo, Kwa ajili umajimaji wake, molases inaweza kuchangwanywa kwenye maji kwa urahisi.n I ngawa inafanya kazi kwa muda mfupi, lakini inasababisha kuongeza uhai wa udongo. Matumizi endelevu ya molases inaongeza viumbe hai kwa asilimia 0.5-1kwa mwaka. Tumia kilichotajwa kwenye 1.
- Inasaidia kupunguza athari za wadudu kwenye udongo (nematodes) iwapo itatumika kwa muda wote wa uzalishaji. Tumia lita 20-25 kwa kiwango katika hekta moja.
- Molases pia husaidia kwenye maeneo yenye tatizo la mchwa na wadudu wanaosafirishwa na mchwa. Kiasi cha kutumia ni kilekile cha lita 20-25 kwa hekta kwa wiki na itumike wakati wote wa kumwagilia.
- Kwa kutumia molases ina asili ya tindikali, inafanya kazi ya kusafisha mipira ya umwagiliaji, mchanganyiko wa lita 25 za molases katika kyubiki mita 10 za maji.
- Kuna dalili kuwa molases inasaidia mizizi kuwa na nguvu ya kufyonza virutubisho katika udongo hasa miziz inapokuwa imekosa maji.
Matumizi ya molases inashauriwa kwa wingi kwa mkulima kwa sababu inafanya kazi ikiwa hai sio sawa na kemikali, na kwa sababu udongo unahitaji ili kuwezesha ukuaji wa mizizi ya mimea, kwa kuweka uwiano wa viumbe hai katika udongo na kuboresha muundo wa udongo unaoruhusu maji kusafiri bila shida. Mizizi yenye afya huwezesha mmea kufyonza virutubisho ardhini na mmea kuwa na afya. Umbile na udongo wenye virutubisho ndio msingi wa uzalishaji bora wa mzao ya mboga na matunda.