Magonjwa yaenezwayo na kupe
Ndigana kali, ndigana baridi, kukojoa damu na moyo kujaa maji.
Kinga: Ogesha wanyama wako kwa kutumia dawa ya kuua kupe mara moja kwa wiki.
Magonjwa yaenezwayo na mbung’o
Ndorobo ni ugonjwa mkuu uletwao na mbung’o
Kinga: Wachanje ng’ombe kwa kutumia dawa iitwayo samorini kila baada ya miezi mitatu.
Magonjwa yasababishwayo na virusi
Ugonjwa wa midomo na miguu, sotoka, ndui
Kinga: Chanjo ya virusi maalum pata ushauri wa daktari wa mifugo
Magonjwa yasababishwayo na bakteria
Chambavu, homa ya mapafu, kimeta
Kinga: Chanjo maalum pata ushauri wa daktari wa mifugo
Lishe duni
Kudumaa, ugumba, mifupa kuwa laini
Kinga: Lisha wanyama chakula kizuri na chenye virutubisho vya kutosha.
Magonjwa yatokanayo na mazingira
Misumari kwenye matumbo, mifuko ya plastiki, kuoza kwato
Kinga: Chambua pumba, toa misumari
Jipu la kiwele
Kinga: Usafi kwenye banda la ng’ombe, kusafisha kiwele kabla na baada ya kukamua. Mkamuaji awe msafi na kucha fupi na aoshe mikono kwa sabuni kabla ya kumkamua ng’ombe. Pata ushauri wa wataalamu wa mifugo kuhusu ugonjwa huu.