Nitrogen
Dalili: Mahindi, maharage na mboga hukua kwa taabu sana, majani yanakuwa na kijani mpauko. Sukumawiki na kabichi majani yanakuwa na mchanganyiko wa rangi ya njano. Majani ya chini ndiyo huathiriwa kwanza, na kiwango cha maua kuchanua hupungua au kuchelewa.
Kutibu: Ongeza kiasi cha kutosha cha mbolea za asili. Panda mimea inayosaidia kuongeza nitrojen kama lablab, desmodium(figiri) na lusina. Weka mboji, samadi na mbolea ya maji yenye nitrojen kwa wingi.
Phosphorous
Dalili: Mahindi, maharage na mbogamboga haikui vizuri. Majani hugeuka na kuwa rangi ya kijani kama bluu na zambarau. Matunda hubakia kuwa madogo. Inaweza kuharibu mizizi au kukosekana kwa Nitrojeni.
Kutibu: Tumia mbolea asili ya maji yenye phosphorus.
Potassium
Dalili: Majani yanakuwa na rangi ya njano kama yanakauka kuzunguka. Kuchanua kwa shida na kutokuwa mpango mzuri wa matunda. Mmea unashambuliwa na magonjwa kirahisi.
Kutibu: Boresha udongo wako kwa kutumia mimea yenye virutubisho vya potassium au weka majivu kwenye shamba lako.