Vyakula vya kuku vinaweza kupatikana madukani au kutengenezwa na mfugaji mwenyewe. Ili kuku aweze kukua haraka na kutoa mazao mengi na bora ni lazima chakula kitengenezwe katika mchanganyiko wenye uwiano mzuri uliopendekezwa.
Chakula cha kuku ni lazima kiwe na viinilishe muhimu kama vile protini, wanga, madini na vitamini. Hakikisha chakula unachotengeneza kina mchanganyiko ufuatao:
- Vyakula vya kujenga mwili kama vile jamii ya kunde, samaki, dagaa, mashudu ya ufuta, pamba na alizeti
- Vyakula vya kulinda na kukinga mwili usipate maradhi kama vile mafuta ya samaki na majani mabichi kama kabichi, mchicha, majani ya mpapai na nyasi mbichi
- Vyakula vinavyojenga mifupa kama vile aina ya madini, chokaa, mifupa iliyosagwa na chumvi. Ukosefu wa vitamini na madini kama Kalishamu na Fosiforasi husababisha matege, kukunjamana kwa vidole, kufyatuka kwa misuli ya goti na kupofuka macho.
Maji ni muhimu sana kwani husaidia kulainisha na kurahisisha usagaji wa chakula, na kupunguza joto. Wakati wa joto kali kuku wapewe maji mengi.
Kabla ya kutengeneza chakula lazima mtengenezaji ajue haya:
- Jinsi ya kupata vyakula vya aina mbali mbali
- Kiasi cha viinilishe vinavyohitajika kwa kuzingatia umri na aina tofauti ya kuku; kwa mfano vifaranga wanahitaji protini asilimia 18 hadi 22, kuku wanaokua asilimia 17 hadi 19 na kuku wa mayai asimilia 15 hadi 17. Vile vile madini aina ya Kalishamu kiasi cha asilimia tatu hadi nne kinahitajika kwa kuku wa mayai na asilimia moja kwa kuku wa nyama na vifaranga.
- Viwango vya uchanganyaji wa aina za vyakula mbali mbali. Ili mtengenezaji aweze kutengeneza chakula bora ni muhimu afuate kiwango cha uchanganyaji
Kilichopendekezwa. Kiasi cha aina moja ya chakula kinapozidi kinaweza kuleta madhara.
Jedwali lifuatalo linaonesha kiwango kinachotakiwa kwa baadhi ya vyakula.
- Vyakula na viwango vinavyohitajika kwa asilimia 100
Aina ya Chakula | Kiwango cha uchanganyaji (%) | ||
Vyakula | Vifaranga | Kuku wa nyama | Kuku wa mayai |
Mahindi | 70 | 70 | 70 |
Ulezi | 20 | 40 | 40 |
Mtama | 20 | 30 | 30 |
Mpunga | 40 | 70 | 70 |
Ngano | 5 | 40 | 40 |
Pumba za mahindi | 10 | 20 | 20 |
Pumba za mpunga | 10 | 20 | 20 |
Pumba za mtama | 10 | 20 | 20 |
Pumba za ngano | 5 | 15 | 15 |
Mashudu ya nazi | 10 | 30 | 40 |
Mashudu ya pamba | 5 | 10 | 5 |
Mashudu ya alizeti | 10 | 20 | 20 |
Mashudu ya ufuta | 10 | 10 | 5 |
Damu iliyokaushwa | 5 | 5 | 5 |
Mifupa iliyosagwa | 5 | 5 | 7.5 |
Dagaa | 10 | 5 | 5 |
Lusina iliyosagwa | – | – | – |
(Lucerne meal) Lukina | 5 | 5 | 5 |
Lcuecana meal | 2.5 | 5 | 5 |
Chokaa | 5 | 5 | 5 |
Chumvi | 0.5 | 0.5 | 0.5 |
Soya | 10 | 20 | 20 |
- Kuhusu kiasi cha viinilishe kama protini, wanga, madini na vitamini vilivyomo kwenye aina za vyakula vitakavyochanganywa, Mfugaji anashauriwa amuone mtaalamu wa mifugo aliyekaribu naye aweze kumpa ushauri zaidi.
- Mchanganyiko uwe na zaidi ya aina moja ya vyakula kwa mfano vyakula vya kujenga mwili vitokanavyo na wanyama na mimea.
- Mfano wa kutengeneza kilo 100 za chakula cha kuku;
Vyakula | Kiasi (Kg) |
Mahindi | 30.00 |
Pumba za mahindi | 20.00 |
Soya | 18.00 |
Mashudu ya alizeti | 20.50 |
Dagaa | 5.00 |
Mifupa iliyosagwa | 4.00 |
Chumvi | 0.50 |
Vitamini | 2.00 |
Jumla | 100.00 |
- Mfano wa chakula cha kukuzia kuanzia juma la nne hadi la nane
Vyakula | Kiasi (Kg) |
Mahindi | 45.00 |
Pumba za mahindi | 20.00 |
Mashudu ya pamba | 5.00 |
Soya | 20.00 |
Dagaa | 2.50 |
Mifupa iliyosagwa | 5.00 |
Chumvi | 0.50 |
Vitamini | 2.00 |
Jumla | 100.00 |
- Mfano wa chakula cha kuku wa mayai kuanzia juma la nane hadi la ishirini
A | B | ||
Vyakula | Kiasi (Kg) | Vyakula | Kiasi (Kg) |
Mahindi | 45.00 | Mahindi | 45.00 |
Pumba za mahindi | 25.00 | Pumba za mahindi | 30.00 |
Soya | 5.00 | Soya | 5.00 |
Mashudu ya alizeti | 10.00 | Mashudu ya pamba | 5.00 |
Dagaa | 4.00 | Dagaa iliyokaushwa | 4.00 |
Damu | 3.00 | Mifupa iliyosagwa | 2.50 |
Chokaa | 3.00 | Chokaa | 3.00 |
Chumvi | 0.50 | Chumvi | 0.50 |
Vitamini | 2.00 | Vitamini | 2.00 |
Jumla | 100.00 | Jumla | 100.00 |
- Mfano wa chakula cha kuku wa mayai kuanzia wiki ya ishirini na kuendelea
A | B | ||
Vyakula | Kiasi (Kg) | Vyakula | Kiasi (Kg) |
Mahindi | 50.00 | Mahindi | 40.00 |
Pumba za mahindi | 15.00 | Pumba za mahindi | 25.00 |
Mashudu ya pamba | 5.00 | Mtama | 5.00 |
Soya | 18.00 | Mashudu ya alizeti | 10.00 |
Dagaa | 4.50 | Dagaa | 4.00 |
Mifupa iliyosagwa | 3.00 | Damu iliyosagwa | 5.00 |
Chokaa | 2.00 | Mifupa iliyosagwa | 4.50 |
Chumvi | 0.50 | Chokaa | 4.00 |
Vitamini | 2.00 | Chumvi | 0.50 |
Jumla | 100.00 | Vitamini | 2.00 |
Jumla | 100.00 |
Habari
Naitwa Fortunatus nipo morogoro, naomba kujifunza jinsi ya kuandaa chakula cha kuku mwenyewe nyumbani Asante.
Habari,
Karibu Mkulima Mbunifu. Ili uweze kujifunza tafadhali soma makala hiyo kwa umakini na ufanye kwa vitendo. Hatuna njia nyingine ya kufundisha zaidi ya kukuandikia makala na wewe kujisomea kisha kufanya wa vitendo.
Karibu Mkulima Mbunifu
Asante kwa ushauri wenu
Karibu sana Mkulima Mbunifu
Naomba ufafanuzi
1. Mfano wa vyakula vya vitamini
2. Soya ni unga au punje kama zilivyo?
Vyakula vunavyowapatia kuku vitamini ni kama vile majani mabichi au mchicha. Soya huwezi kulisha kuku moja kwa moja kama maharage kwani yana kizuizi cha kimeng’enyo kijulikanacho kama trypsin hivyo mashudu ya soya hutumika na siyo maharage yenyewe.
…assnte kwa elimu, ila nimeona hapo kwenye uchanganyaji wa chakula, umeweka mahindi kwa kila rika, ila sijaona kuhusu vifaranga wa siku 1 na kuendelea unachanganyaje maana wale wanahitaji mash
Kwa vifaranga wa siku moja mpaka miezi miwili
Unga wa dona wa mahindi au mtama kg 40
Pumba za mtama, mahindi au uwele kg 27
Mashudu ya alizeti, ufuta, pamba au karanga kg 20
Unga wa mifupa au chokaa ya kuku kg 2.25
Dagaa au mabaki ya samaki kg 10
Chumvi 0.5
Premix 0.25
Jumla utapata kilo 100
Unapoesema mahindi soya, na dagaa huo mchanganyo badae unausaga kwa pamoja ua unachanganya bila kusaga??
ASante kwa mafonzo yenu
Habari, Karibu sana Mkulima Mbunifu na usisite kuwasiliana nasi
Huu
Karibu Mkulima Mbunifu, hapa tunajishughulisha na utoaji wa elimu ya uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo kwa misingi ya kilimo hai/ kilimo endelevu/ kilimo ikolojia na kwa njia ya majarida ambayo hutumwa nakala ngumu kwa wakulima waliokjo kwenye vikundi na kwa wale wasio na vikundi kuweza kutumia kwa njia ya kimtandao kama barua pepe au whatsapp.
Karibu sana kwa swali au maoni
Karubu tujifunze zaidi
Na Mimi naitwa DIEGO ASUKULU nipo Congo, naitaji mafundisho ya kutengeza chakula cha kuku na utunzaji wa kuku ya kizungu (pondeuse) hivyo kuku nilizo nazo tayari zinaanza fariki, kwa msaada wenu nitashukuru
Habari,
Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa swali lako. Kuhusu jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku soma hapo kwenye makala tumeandika kila kitu hatua kwa hatua lakini kuhusu hao kuku unaosema wa kizungu sisi hatujawafahamu bado
Asante sana kwa elimu nzuri
Karibu sana
Simkoko.
Nataka kulima pilipili hoho(paprika). Procedures kuanzia kitalu mnazo?
Habari, Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kufuatilia na kusoma makala zetu.
Kwa kilimo cha pilipili hoho (Capsicum) na siyo paprika, tutalifanyia kazi na kuandaa makala husika.
Hello sasa Nita pata wapi solo ya pilipili hoho?
Habari, karibu Mkulima Mbunifu na aante kwa kufuatilia na kusoma makala zetu. Unaweza kununua kwenye maduka ya pembejeo za kilimo nchini kote, sisi hatuuzi
Kuna uhusiano baina ya lishe husika na jamii ya kuku yaani kama ni kuchi atakua tofauti na aina nyingine ya kuku kwenye lishe zao?
Habari, karibu Mkulima Mbunifu.
Hakuna tofauti kwenye lishe kwa kuku aina zote, lishe inakuwa tofauti tu kwa vifaranga na kuku wakubwa na hasa kwa vipimo na uandaaji wa chakula husika.
Nimejifunza kutengeneza chakula chakuku hakika Nita win
Habari, Karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala zetu. Tunafurahi kusikia kuwa umejifunza na kufanya kwa vitendo kile tulichokieleza na hata sasa unafurahia mafanikio yako. Tafadhali tunaomba utupatie namba yako ya simu
Good
Thanks
good
Helpful knowledge, thanks so much!
Thank you very much, you are mostly welcome and in any query do not hesitate to contact us
There whatsup group please? Can we get a link to join
Habari, Karibu san Mkulima Mbunifu. Kwa whatsapp tunapatikana kwa namba 0717 266 007
Jamani mm sijaelewa jinsi gan ya kutegeneza hayo majani ya mpapai unampa kuku ivyo ivyo au una ya kausha juani kwanza au una ya fanyaje?
Habari,
Majani ya papai ni unawapa kuku wanakula kwa kudonoa kama wanavyokula majani mengine kama mbogamboga au kama utaweza kukata vipande vidogovidongo sana unakata unawapa wanakula.
Karibu
Asanteni sana kwa Elimu ya kutengeneza chakula cha kuku. Kama kuna watu wametumia huu mchanganyiko wa vyakula vya kuku wa mayai – tungeshukuru sana kama wangetoa mrejesho nyuma humu kwenye tovuti yenu.
nimefurahia mafundisho; endelea kuelimisha
Karibu sana Mkulima Mbunifu
samahan naomba kuuliza,je huo mchaganyiko wa vyakula vya kuku vinachaganywa kwa mashine?,je hiyo mashine inagharimu shigapi? Asanteni
Habari, kama una mashine utachanganya kwa mashine kama huna utachanganya tu kwa mikono mpaka ichanganyike vizuri
Aanteni sana kwa elim hii ila naomba kujua je kuku wa kienyeji mchanganyo wa chakula chao unakuwaje? ukianzia vifaranga hadi anaeetaka kutaga. na chakula cha kuwakuzia ni kipi au kinaandaliwa vipi?
Habari, mchanganyiko huu wa chakula tulioandika ndiyo huo huo unaweza kuutumia kwa kuku wa kienyeji hasa, inategemea sasa kama unahitaji kuku wako wajenge nyama sana au watage mayai kwa wingi hivyo kama unahitaji kuku wajenge nyama basi tumia mchanganyiko wa nyama na kama ni unahitaji mayai basi tumia mchanganyiko wa kuku wamayai. Karibu sana
Habari mkulima mbunifu ahsante kwa elimu yenu nzuri na wasiwasi kwa kutumia malighafi ya nyumbani ili nipunguze gharama za kwenda dukani kwenda kununua chakula cha kuku nilikuwa naomba kuuliza kwenye mahindi na soya je hapo ni tunawapa kama ilivyo ama ni ni kuparaza then tunapima ndo kuwapa kuku ama ntakushuru sana kwa majibu yako mazuri
Soya huwezi kulisha kuku moja kwa moja kama maharage kwani yana kizuizi cha kimeng’enyo kijulikanacho kama trypsin hivyo mashudu ya soya hutumika na siyo maharage yenyewe.