- Binadamu, Mifugo, Samaki

Je, Una swali lolote kuhusiana na ufugaji wa Samaki? Tuulize, Tukujibu

Sambaza chapisho hili

Ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa MkM kuthamini maoni yako na kujibu maswali yenu kwa kupitia wataalamu wa kada mbalimbali.

Katika toleo hili Musa Said ambaye ni mtaalamu wa Samaki anaendelea kujibu maswali kuhusiana na ufugaji wa samaki. Shime, kama nawe una maswali basi usisite ili upate jibu na uondokane na dukuduku.

Lai otieno anauliza: Mimi natoka Musoma mjini na nataka kufuga samaki kwa njia ya kisasa, Je, bwawa naweza kuweka mbali na maeneo ya ziwa au jirani na ziwa. Pili, kuna uwezekano wa kutumia maji ya bomba?

Musa Said anajibu: Itakuwa vizuri ukiweka umbali usiopungua mita 10. Inawezekana pia kutumia maji ya bomba, cha msingi hakikisha yasiwe na kemikali, ingawa ni vizuri zaidi maji hayo yakiwa yamepimwa na wataalamu. Ahsante.

Jonathan anauliza: Mimi nakaa kigamboni maeneo ya mwembe mdogo na eneo langu lina udongo wa mfinyanzi sehemu kubwa na maji yapo karibu sana, ukichimba nusu mita unakutana na maji mengi. Pia nina kisima cha kupandisha na mota cha mita 50, maji yake ni baridi (hayana chumvi hata kidogo na ni mengi), Je, uchimbaji wa bwawa la samaki unahitaji kusakafia kwa sementi? Je, makadirio ya uchimbaji bwawa sehemu kama hii inaweza kugharimu kiasi gani kitaalamu? Pia, samaki aina ya sato dume anauzwaje kwa kifaranga (huko juu ulisema kwa pelege, au pelege ndo satto?). Pia ulisema, ufugaji wa semi extensive unaanzia samaki wa 4-10 kwa square mita moja, Je, kwa sato dume unaweza kufuga samaki 10 kwa squre mita moja? Nikitaka kufanya ufugaji huu kuwa ndiyo biashara yangu ya uzalishaji, Je, unaweza kunipa mchanganuo na faida yake, kwa mfano ukianza na samaki 2000?

Musa Said anajibu: Uchimbaji wa bwawa la kufugia samaki sio lazima lijengewe kwa simenti, kikubwa sana tunachokizingatia ni uthibiti wa maji ndani ya bwawa usipungue chini ya mita moja au moja nusu. Na hii ni kulingana na tabia ya eneo lako la mradi likoje na linahitaji bwawa la aina ipi. Gharama za uchimbaji kwa kweli  hazipo maalumu kulingana sehemu husika, mara nyingi tunakupigia gharama baada ya kuona eneo lako lipoje na pia mradi wako unataka uwe wa ukubwa gani, na mambo mengine mengi ambayo tutayadadisi kwenye eneo lako na baadae kukupa gharama halisi ya kitaalamu. Gharama         ya sato dume ni Tsh 200 tu. Kuweka samaki 10 kwa mita moja ya mraba inawezekana lakini lazima mtaalamu uwe nae karibu sana kwani uwekaji kwa wingi ndani ya bwawa unahitaji umakini na uelewa wa hali ya kumtambua samaki anataka nini, kwanini, kwa wakati gani, na ufanye nini.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

2 thoughts on “Je, Una swali lolote kuhusiana na ufugaji wa Samaki? Tuulize, Tukujibu

Leave a Reply to M MAPULI Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *