- Mifugo

Aina bora ya nguruwe kwa ajili ya kufuga

Sambaza chapisho hili

Nchini Tanzania, ufugaji wa nguruwe unazidi kuongezeka siku hadi siku. Hii ni kwa sababu nguruwe ni moja kati ya mifugo inayompatia mfugaji kipato kwa haraka, kwani huzaa mara mbili kwa mwaka na kila mzao anaweza kuzaa watoto 12.

Pamoja na matunzo mengine ya nguruwe ili mfugaji aweze kupata faida kama alivyokusudia, ni muhimu kufahamu sifa za nguruwe bora wa kufuga.

Sifa za nguruwe bora.

Dume

  • Asichaguliwe kutoka kwenye ukoo wenye historia ya magonjwa au kilema cha kurithi.
  • Awe na miguu imara, mchangamfu na mwenye afya bora.
  • Awe na umbile zuri na misuli imara itakayomuwezesha kupanda bila matatizo.
  • Awe mwenye kende zilizokamilika.
  • Awe anayekua haraka na mwenye uwezo mkubwa wa kubadili chakula kwa matumizi ya mwili kuwa nyama.

Jike

  • Awe na umbile la kumuwezesha kubeba mimba na kuzaa kwa urahisi.
  • Awe na chuchu zisizopungua 12 na ziwe zimejipanga vizuri.

Aina za nguruwe

Kuna aina nyingi za nguruwe wafugwao; zifuatazo ni  baadhi ya aina zinazofugwa nchini Tanzania;

  1. Nguruwe mkubwa mweupe (Large White)
  • Ni mweupe, masikio yake yamesimama na paji la uso limeingia ndani kama bakuli.
  • Si rahisi kushambuliwa na magonjwa.
  • Wenye umri mdogo, nyama yake haina mafuta mengi.
  • Hukua na kuongezeka uzito kwa haraka sana.
  • Jike hutoa maziwa mengi.
  • Dume hutumika kwa ajili ya kuboresha aina nyingine za nguruwe.

 

 

 

 

 

 

 

  1. Nguruwe Mrefu Mweupe (Landrace)
  • Aina hii ya nguruwe ni mrefu mweupe na mwembamba kuliko yule mkubwa mweupe.
  • Masikio yake yameinama kwa mbele.
  • Haongezeki uzito upesi na hutoa nyama isiyo na mafuta mengi.
  • Aina hii ikipandishwa na aina ya kwanza huzaa nguruwe anayetoa mnofu mzuri zaidi usiokuwa na mafuta mengi.

 

 

 

 

 

 

 

 

  1. Nguruwe mfupi mweusi mwenye mstari mweupe kuzunguka mwili kwenye miguu ya mbele (Wessex Saddleback)
  • Masikio yameinama.
  • Mgongo umepinda kidogo mfano wa upinde.
  • Hutoa mafuta mengi sana.
  • Hutoa maziwa mengi, huzaa watoto wengi na kuwatunza vizuri.
  • Ni uzao unaotokana na kupandisha nguruwe wa aina tofauti.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

  1. Nguruwe chotara
  • Nguruwe wa kienyeji akipandishwa na wa kisasa.
  • Anastahimili magonjwa, anakua haraka na nyama yake huwa haina mafuta mengi.
  • Anastahimili mazingira magumu kuliko wa kisasa.
  1. Nguruwe wa kienyeji
  • Huwa ni wadogo kwa umbo.
  • Wanakuwa taratibu hata kama wanapatiwa chakula bora.
  • Hawana rangi maalumu.
  • Hustahimili mazingira magumu.
  • Nyama yake haina mafuta mengi.
  • Wana uwezo wa kujitafutia chakula.

Kwa maelezo zaidi juu ya ufugaji wa nguruwe, unaweza kuwasiliana na mtaalamu wa mifugo kutoka SUA; Agustino Chengula kwa simu +255767605098

 

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

49 maoni juu ya “Aina bora ya nguruwe kwa ajili ya kufuga

  1. Hongereni kwa machapisho yenu yana tusaidia sana,ila mna wasaidiaje wakulima kupata mbegu bora za mifungo??

    1. Asante sana kwa kuwa msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu. Ni kweli mara nyingi tunawasaidia kwa kuwaunganisha na wafugaji wanaouza mifugo yao yenye ubora lakini pia kwa kununua mbegu kutoka katika shamba la serikali. Karibu sana

        1. Habari, Karibu Mkulima Mbunifu

          Hongera kwa hatua hiyo ya kwanza ya kupata mtaji na kuamua kutaka kuingia kwenye ufugaji wa nguruwe.

          Kuhusu kupata mbegu mbora kama una uwezo wa kusafirisha kutoka mikoani tutakuunganisha na wauzaji wa mbegu bora kutoka Arusha lakini kwa huko Rorya kwasasa hatuna uhakika wa wauzaji wa mbegu bora. Unaweza pia ukatupigia kwa simu namba 0717 266 007 kwa ushauri zaidi.

          Karibu

          1. Naaam, habari
            Nami niko mbeya napataje mbegu ile ya large white na ile ya land race, msaada tafadhari

          2. Habari, karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kufuatilia na kusoma makala zetu.
            Tafadhali wasiliana na Nelson Kesyy kwa simu namba 0713 948 144

          3. Habari niko dsm naomb connection ya kupata pure landrace kwa uku dar nahitaj wa kufuga

          4. Habari, Karibu Mkulima Mbunifu. Tfadhali wasiliana na Bw. Uledi Kimbavala kwa simu namba0768 864 628

      1. Nimefurahi kusikia kuna kuunganishwa nasehemu ambazo zinaaminika
        Kwamfano mimi Niko mbeya mnaweza kuniunganisha sehemu ambayo nitaweza kupata Mbegu nzuri za ngurue

        1. Habari,
          Karibu sana Mkulima Mbunifu na tunashukuru kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za jarida letu.

          Wasiliana na Nelson Kessy kwa simu namba 0713 948 144

          Karibu

        1. Habari, Karibu Mkulima Mbunifu.
          Nguruwe hawa wanapatikana kwa wafugaji, sisi Mkulima Mbunifu hatuuzi ila tunaweza kukuunganisha na wafugaji ukanunua kutoka kwao. Sisi tunapatikana Arusha

    1. Naitwa Kubache Cheketela.
      Napatikana :kakola- kahama Mkoa wa SHinyanga.
      Naomba kuuliza ni aina ipi ya nguruwe ambao ni bora kwa biashara na wanahitajika sana Sokoni kulingana na uzoefu wako mkulima mbunifu? Na naweza kuwapata wap?

      Mimi nahitaji kufuga nguruwe kwa biashara, naomba msaada wa ushauri wenu.

      Napatikana kwa :0678966640
      Whatsap: 0766146640.
      Email:Kbathromew@gmail.com

  2. Hongereni sana kwa majalida mazuri ya ufugaji wa nguruwe,,,
    Ningependa kuuliza kwamba je kama mfugaji anafuga nguruwe wa kienyeji na anataka wakue kwa haraka zaidi je anaweza kuwapatia mchanganyiko bora wa virutubisho vyote au atafanyaje

    1. Habari Bw.James
      Karibu sana Mkulima Mbunifu na tumefurahi kusikia kuwa unayapokea majarida yetu na umefurahia elimu itokanayo na majarida haya. Hongera sana na endelea kufuatilia makala zetu za kila mwezi bila kukosa.
      Kuhusu chakula cha bora kwa ajili ya nguruwe wako tafadhali wasiliana na Abrogast Msangawale kwa simu namba 0785 000777

      Karibu sana Mkulima Mbunifu

          1. Habari, Karibu Mkulima Mbunifu
            Naomba uliweke swali lako vizuri, unaposema shamba la serikali ni la kufanyaje, la kununua ama shamba la maonyesho la mazao, ama linalomilikiwa na serikali ama la aina gani?

          1. Habari, karibu Mkulima Mbunifu. Ngoja tuulize kwa wauzaji. Unapatikana mkoa gani

      1. Kuna amina ya ngurue anaezaa watoto mpaka 20.anapatikana wapi na ni amina gani ?

          1. kwa wakazi wa mkowa wa kilimanjaro wanawezaje pata ngurue bora kwa kufuga

          2. Habari,

            Karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala zetu. Unaweza kuwapata ila kwasasa tuna mawasiliano na muuzaji toka Arusha ambaye anaweza pia kukusafirishia kwa gharama mtakazokubaliana nazo.

            Wasiliana na Nelson Kessy kwa simu namba 0713 948 144

            Karibu sana Mkulima Mbunifu

  3. Nashukuru sana kwa makala yenu, je nitapataje mbegu Bora kwa ajili ya ufugaji was kibiashara?? Na je ni virutubisho gani nguruwe anatakiwa apewe ili akuwe kwa haraka zaidi?

    1. Habari Sia. Karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa swali lako kwetu.
      Kuhusu mbegu bora kuna wauzaji wengi wanaouza mbegu na hata virutubisho kwa ajili ya kuwalisha nguruwe na kuongezeka na kukua kwa haraka zaidi.

      Unaweza kuwasiliana na Aborgast Msangawale kwa simu namba 0785 000 777 kwa msaada zaidi.

      Unaweza pia kusoma kuhusu chakula cha kukuzia kwa kubonyeza hapa https://mkulimambunifu.org/mifugo/chakula-rahisi-kwa-utunzaji-wa-nguruwe-wadogo-wanaokuwa/

      Karibu sana Mkulima Mbunifu.

  4. Nataman nianze kufuga nguruwe ila bado sijapata jibu la swali langu kuwa nifuge wa Aina gan ili ninufaike

    1. Habari Stephano. Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa swali lako.
      Kuhusu aina ya nguruwe wa kufuga soma vizuri makala hii tumeeleza vyema ni wewe tu kuamua unataka kufuga yupi kutokana na sifa zake na sifa unazozihitaji pia.

      Karibu sana MkM

  5. Habari na poleni kwa majukumu.
    mimi naitwa Raymond, nipo Wilaya ya Kasulu-Kigoma. Nahitaji kuanzisha mradi wa ufugaji Nguruwe ila sijajua kwa huku nilipo kama naweza kufikishiwa mbegu bora za nguruwe na gharama yake ipoje.
    Nawasilisha kwa msaada zaidi wa kuunganishwa na wafugaji wanaouza mbegu bora na wenye uwezo wa kufanikisha jambo hili.

    1. Habari Raymond,
      Karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za jarida la Mkulima Mbunifu.

      Ili kuweza kupata mbegu na hata ushauri wasiliana na Bw. Lukumay kwa simu namba 0753 739174

      Karibu sana

  6. Mm cjui kutofautisha mbegu za kisasa na kienyej na nawezaje kupata mbegu nzur na za muda mfupi?

    1. Habari,

      Namna ya kutofautisha ni kama tulivyokueleza kwenye makala hii, soma vizuri kwa kutulia utaelewa na kama hujaelewa bado mtafute mtaalamu wa mifugo aliyekaribu na wewe ili akusaidia kutambua tofauti zao. Pia hakuna nguruwe wa muda mfupi ila uzalishaji wa mazao ya nyama ndiyo umetofautiana kama ambavyo tumeeleza hapo juu. Hivyo unaweza ukachagua aina mojawapo hapo juu kwa kuangalia sifa zake na uzalishaji wake

      1. Nashukuru kwa makala nzuri. Nataka kuanzisha mradi wa nguruwe. Lakini nipo buseresere chato sijui ntawezaje kupata mbegu bora nitakayonufaika nayo. Na maelezo zaidi

        1. Karibu sana Mkulima Mbunifu.

          Kwa masaada zidi wasiliana na mtaalamu wa mifugo kutoka SUA; Agustino Chengula kwa simu +255767605098

  7. Makala nzuri sana. Nngependa kujua suala la mabanda mazuri ya kisasa ya kufugia nguruwe yakoje na gharama zake

    1. Habari,

      Mabanda yanatengenezwa na gharama hutegemea ukubwa wa mabanda na aina ya banda linalotengenezwa.

  8. Nimefurahi kukutana na makala hii nzuri,mimi nimeanza ufugaji huo lakini sikuwa na darasa la helewa .matarajio yangu ni kuwa na shamba kubwa la nguruwe.kupitia hapa naamini nitajifinza mengi.
    Aliyeniuzia nguruwe alinipa dume large white na jike landress .

    1. Habari, Karibu Mkulima Mbunifu na tunafurahi kwa kujiunga kwako na mtandao wetu wa elimu. Tuko tayari kukusaidia pale utakapokuwa naswali na kukushauri kadri ya uwezo wetu. Karibu sana

  9. Ni mara ya kwanza kufuatilia makala zenu nimependa pia nashukuru kwa kunipa uelewa,Mimi ninaomba kupata elimu ya kuandaa mchanganyiko sahihi wa chakula Cha nguruwe kuanzia hatua ya awali mpaka mwisho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *