- Mifugo

Chakula cha nguruwe kinahitaji virutubisho sahihi

Sambaza chapisho hili

Nguruwe huhitaji kulishwa vizuri ili waweze kukua haraka na kufikia uzito wa kuchinjwa mapema. Ikiwa watatunzwa vizuri watafikia uzito wa kilo 60 hadi 90 wakiwa na umri wa miezi sita hadi tisa

Nguruwe ana uwezo wa kula vyakula vya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na mabaki ya vyakula vya nyumbani, shambani na viwandani.

Pamoja na vyakula hivyo, ni muhimu kumlisha chakula cha kutosha, bora na chenye viinilishe vyote vinavyohitajika mwilini. Hata hivyo ili kupunguza gharama mkulima anashauriwa kumlisha vyakula vinavyopatikana katika mazingira yake.

Mfugaji anaweza kuchanganya chakula mwenyewe au kununua kutoka kwenye maduka yanayouza vyakula vya mifugo. Mchanganyiko huo uwe na makundi muhimu ya vyakula kwa ajili ya nguruwe.

Makundi ya Vyakula Kuna makundi makuu matatu ya vyakula ambavyo ni;

Vyakula vya kujenga mwili.
Hivi vinahitajika mwilini kwa ajili ya kuimarisha misuli na kujenga mwili kwa mfano maharage, soya, mashudu ya pamba, alizeti, ufuta na nazi. Vyakula vitokanavyo na wanyama kama mabaki ya nyama, damu, dagaa au samaki
na maziwa yaliyokaushwa.

Vyakula vya kutia nguvu na joto
Vyakula vya nafaka kama vile ulezi, ngano, mahindi, mpunga, pumba na mabaki ya vyakula mbali mbali kama mikate, viazi, mihogo na machicha ya pombe.

Vyakula vya kulinda mwili (madini na vitamini)
Kundi hili linajumuisha madini kama mifupa iliyosagwa, chokaa, unga wa maganda ya mayai, chumvi na vitamini kama majani mabichi, mchicha, maboga na matunda.

Maji
Pamoja na kupewa chakula, maji safi na ya kutosha ni muhimu ili chakula kiweze kutumika vizuri mwilini. Nguruwe anahitaji maji wakati wote

Mahitaji kwa ajili ya kutengeneza chakula cha nguruwe;
• Chumvi paketi tatu (3)
• Pumba ya mchele kilo 110
• Unga wa soya kilo 16.5
• Mashudu kilo 11
• Karboni gramu 3.3 (ina Kalsiamu, inasaidia mmengenyo wa chakula na kuondoa gesi)
• Molasis mililita 440 (ina kinga magonjwa na kuzuia harufu mbaya)
• Maji lita 46.5
• Molasis mililita 440
• EMAS – (Effective Micro-organisms) mililita 440
• FFJ- (Fermented Fruit Juice) au
• FAA- (Fish Amino Acid) lita 3, hii ina omega 3.

Jinsi ya kufanya
Changanya vizuri mahitaji tajwa na hifadhi mahali pakavu kwenye mfuko tayari kwa matumizi ya nguruwe.

Muhimu: Hakikisha unazingatia uwiano sahihi wa chakula kwa kila hatua ya ukuaji wa nguruwe.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *