Tanzania ina uwezo mkubwa wa ufugaji wa ng’ombe wa nyama jambo ambalo linaweza kupelekea wakulima wadogo kupata fedha ikiwa watafanya usimamizi wa hali ya juu kuzalisha nyama kwa muda mfupi.
Hata hivyo, malisho na maji bado ni changamoto kwa ufugaji wa ng’ombe wa nyama nchini kwani nyasi huwa nyingi wakati wa msimu wa mvua na hupunguka wakati wa kiangazi.
Ili kuwaweka wanyama katika hali nzuri kwa mwaka mzima, wafugaji wa nyama lazima wahifadhi nyasi na aina zingine za malisho na kuweka idadi ya wanyama.
Usimamizi
Waogeshe mara kwa mara ili kuepukana na magonjwa yaenezwayo na kupe pamoja na ndorobo. Uogeshaji unaweza kufanyika kwa kutumia pampu za mgongoni (knapsack sprayers) au kuwatumbukiza katika josho lililotiwa dawa ya kuogeshea.
Wape dawa za minyoo mara kwa mara ili kuhakikisha ukuwaji wao unaendelea vizuri. Wape dawa hii kila baada ya miezi mitatu
Wape ndume namba au alama za utambulisho mara wafikiapo miezi 6 tangu kuzaliwa. Utambulisho unaweza kuwa wa chuma au plastiki chenye nambari kwenye sikio, mikato maalumu katika masikio au chapa katika sehemu maalum za mwili.
Ulishaji
Lengo kuu ya ulishaji wa ng’ombe wa nyama ni kuongeza kasi ya kukua na kuongeza uzito kwa haraka. Mfugaji asitegemee tu malisho peke yake ambayo hayawezi kukidhi mahitaji ya lishe hasa katika miezi ya mwisho kabla ya kuuza ng’ombe kwa soko.
Nyasi ni chakula cha gharama ya chini kwa ulishaji wa ng’ombe. Kwa mfumo huria, wapeleke kwa ndume kwa malisho na kama hauna eneo la malisho basi nyasi iliyokatwa na hifadhiwa (hay). Wapate ya kutosha. Kwa kawaida, ng’ombe wanalishwa vipimo sawa na 3% ya uzani wa mwili. Ng’ombe wa kilo 250 atahitaji angalau kilo 9 ya hay. Na kama unamlisha nyasi ya Napier basi atahitaji angalau kilo 50. Pia, ongeza mikunde kama vile desmodium, lusina, au majani ya miti kama kalindra ambazo ni vyanzo vya protini.
Sileji ni chakula chenye nguvu na inaweza kutumiwa baadaya ya ndume kutoka kwenye malisho. Ng’ombe wa kilo kilo 250 atahitaji angalau kilo 20 ya sileji. Uamuzi wa kulisha sileji kwa wanyama wa nyama hutegemea na gharama ya uzalishaji wake. Ikiwa gharama ni ya juu, basi achana nayo.
Lisha chakula cha ziada ili kukidhi mahitaji ya kukua kwa haraka na kujaza nyama kwa muda wa miezi 3 – 6 kabla ya kuchinjwa. Nunua au fanya mchanganyiko wako mwenyewe shambani kulingana na malighafi. Cha muhimu ni chakula chanzo cha nguvu mwilini. Unaweza kuchanganya ifuatavyo;
Malighafi | Kiasi (Kilo) |
Mahindi (iliyosagwa au pumba) | 67 |
Mashudu ya alizeti/pamba | 20 |
Unga wa soya | 10 |
Chokaa ya mifugo | 2 |
Chumvi | 1 |
Jumla | 100 |
Kumbuka chakula cha ziada inatumika kunenepesha kabla ya kuuza ili kufikia uzito wa kilo 300-400. Hivyo, hakikisha unanenepesha ndume ambaye amefikisha angalau kili 250. Ndumu huyu atahitaji chakula cha ziada kilo 3-6 kwa siku. Wanyama wanaolishwa kwa njia hii hutoa nyama bora laini, yenye ladha nzuri. Ukilisha chakula cha ziada kwa muda mrefu, gharama itakuwa juu na faida kupungua.
Sehemu ya kulishia
Haijalishi ukubwa wa shamba lako, kutumia mfumo maalum wa kulisha itakusaidia kwa njia nyingi hasa unapowalisha ndume wako chakula cha ziada. Ukijenga mabwawa ama chombo cha kulishia, malisho hayatapotea wakati wanapewa, na ng’ombe watazoea baada ya muda. Unaweza kujenga ukitumia mbao, chuma, ama matofali na saruji. Italingana na uwezo wako kifedha. Ukubwa wake itategemea idadi wa ndume unaowalisha.
Kwa kutumia mabwawa ya kulisha, utapata kulisha wanyama kadhaa kwa wakati mmoja na uamue ni nini au ni kiasi gani cha chakula kinaongezwa kwenye chombo hicho ili uweze kudhibiti kiasi ya malisho ambayo wanaweza kula. Zaidi, zitakusaidia kuweka shamba lako likiwa limepangwa na kukurahisishia kuweka rekodi ya ulaji wa ndume wako.
Vifaa vya maji
Ng’ombe wapatiwe maji safi na ya kutosha. Uchafu unaweza kusumbua shughuli za mmeng’enyo wa chakula au kusababisha maradhi. Maji yakiwa baridi sana, ng’ombe watashindwa kunywa ya kutosha. Jenga birika ya kunywa maji ili kupunguza maji kupotea. Upana bora ni karibu sentimita 20. Hii inaruhusu wanyama kunywa kwa urahisi na hupunguza hatari ya wanyama kuanguka ndani ya birika.
Mpango wa afya
Ndume hawapendi kusumbuliwa, kwa hivyo washughulike kwa uangalifu. Kuwa na daktari wa mifugo karibu ili kuwakagua mara kwa mara hasa ndume wapya kabla ya kuchanganya na ndume wengine. Wape chanjo dhidi ya magunjwa sugu katika maeneo yako na dawa dhidi ya vimelea vya ndani kama minyoo. Kupe na ugonjwa wa ndigana ni moja wapo ya tishio kubwa kwa ng’ombe.
Hongera sana nimepata kitu chakuongeza kwenye ufugaji wangu, asante
Asante na karibu Mkulima Mbunifu tujifunze sote
Darasa zuri sana natengemea kuanza ufugaji wa hivyo mmeniongezea kitu
Karibu sana tuko pamoja kushirikishana uzoefu na kupata elimu zaidi.
nahitaji ng,ombe aina ya boran kwajili ya unenepeshaji
nahitaji ng,ombe aina ya boran kwajili ya unenepeshaji nipo igunga
nahitaji ng,ombe aina ya boran kwajili ya unenepeshaji nipo igunga
Habari
Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa swali lako. Kuhusu ng’ombe wa aina hii ngoja tukuulizie lakini kwasasa hatuna uhakika ni wapi unaweza kuwapata.
Asante sana kwa somo hili la faida… Mungu abariki kazi ya mikono yako.
Karibu sana Mkulima Mbunifu
Nategemea kuanza ufugaji wilaya ya Bagamoyo. Huku maji ni ya chumvi chumvi. Je yanafaa kwa ufugaji?