Mara tuu baada ya kuzaliwa na kwa kipindi cha siku 3 hadi 4 za mwanzo, ndama huhitaji maziwa ya mwanzo ya mama yake yaani dang’a (colostrum) Ni jambo la muhimu sana kuhakikisha kuwa baada ya kuzaliwa ndama anapata maziwa haya ya mwanzo kabla yakupita masaa mawili.
Faida ya maziwa ya mwanzo
- Maziwa ya mwanzo yana kiwango kikubwa zaidi cha viinilishe ukilinganisha na maziwa ya kawaida.
- Viinilishe ambavyo huwemo kwenye maziwa ya mwanzo kwa kiwango kikubwa zaidi ni aina mbalimbali za vitamini na madini pamoja na viini vya kinga dhidi ya maradhi.
- Maziwa haya humpa ndama uwezo wa kupambana na magonjwa yanayoathiri sana ndama wadogo.
- Husaidia ndama kutoa kinyesi cha kwanza (meconium) kutoka tumbo la ndama, kwani ina utelezi.
- Iwapo kwa bahati mbaya ng’ombe/mbuzi mzazi atakuwa amekufa kabla ya ndama hajapata maziwa ya mwanzo, inashauriwa kumpatia maziwa ya mwanzo kutoka kwa ng’ombe/mbuzi mwingine aliyezaa wakati huo.
- Ni lazima maziwa ya mwanzo yapatikane na yanyweshwe kwa ndama huyo ili aendelee kuishi na kukua akiwa na afya.
- Kama itakuwa ni vigumu kupata maziwa ya mwanzo, utaratibu ufuatao utatumika ili kutengeneza maziwa ya mwanzo mbadala.
Namna ya kutengeneza maziwa mbadala ya dang’a
Vitu vitakavyohitajika
- Yai bichi zima 1
- Maji safi ya uvuguvugu lita 1
- Mafuta ya samaki kijiko 1
- Mafuta ya nyonyo (castor oil) vijiko vya chai 3
Namna ya kutengeneza
- Changanya vipimo hivyo kwa usahihi, weka kwenye chombo kisafi cha kunyweshea na kisha mnyweshe ndama
- Hakikisha mchanganyiko huo unakuwa bado wa uvuguvugu unapompa ndama
- Ndama apewe mchanganyiko huo mara tatu (3) kwa siku kwa muda wa siku nne (4) za mwanzo wa maisha yake, baada ya siku nne (4) endelea na unyweshaji wa maziwa ya kawaida ya ng’ombe/ndama
- Wiki 2 ndama aanze kupewa majani malaini pamoja na pumba kidogo, hakikisha anakuwa na maji safi ya kunywa kwenye chombo chake wakati wote
- Ndama aachishwe kupewa maziwa akiwa na umri wa miezi 3
- Mfugaji ahakikishe ndama anaeachishwa anakuwa na afya nzuri
Muhimu:
Vyombo vinavyotumika kulishia ndama visafishwe vizuri kwa
Maoni kupitia Facebook