- Kilimo

Yafahamu magonjwa ya mimea ili kuyadhibiti

Sambaza chapisho hili

Mkakati mzuri kwa wakulima wanaozingatia ikolojia ni kujifunza na kuelewa sababu ya magonjwa, athari zake ili kuweza kukabiliana nayo. Hii inasaidia kulinda mazao ya mimea, kudumisha usalama wa uzalishaji wa chakula.

Kwa kawaida, ni ngumu kuzuia ama kurekebisha tatizo ikiwa haujaelewa tatizo lenyewe. Ndio maana wakulima wanashauriwa kuwa makini shambani kutambua kwa haraka uvamizi wa wadudu na pia magonjwa.

Maana rahisi ya magonjwa ya mimea ni kuwepo kizuizi, au usumbufu fulani unaosababishwa na magonjwa. Kutokana na sehemu ya mmea kupata usumbufu huo, seli za mmea zinaweza kufa au hata kusababisha mmea kufa kabisa. Jambo hili kwa kawaida husababisha kuathirika kwa kiwango cha mavuno, au kuwa na mavuno yasiyokuwa na ubora.

Magonjwa ya mimea yanaweza kugawanywa katika makundi mawili:

  1. Magonjwa yanayosababishwa na vimelea vya nje, au yanayosababishwa na vimelea wengine kama vile fangasi, bakteria, virusi na minyoo inayoshambulia mimea.
  2. Magonjwa yasiyosababishwa na vimelea (yasiyotokana na maambukizi). Dalili zake hutokana na sababu mbalimbali, hii ni pamoja na madhara yanayotokana na madini, kutokuwepo na uwiano wa virutubisho, kukosea wakati wa kuvuna na kuhifadhi, vichocheo vinavyotokana na mazingira, kwa mfano, uchafuzi wa mazingira na madhara yanayotokana na dawa za kuulia magugu.

Sababu ya magonjwa

Magonjwa yote yanayosababishwa na vimelea ni matokeo ya mwingiliano wao na mimea husika, na sababu nyingine za kimazingira kama vile mwanga, joto, na unyevu. Mwingiliano huu hujulikana kama mzunguko wa magonjwa wa pembe tatu. Endapo sehemu moja wapo katika mzunguko huu itakosekana, basi ugonjwa hautakuwepo.

Kimsingi mlipuko wa magonjwa unategemea sababu tatu;

  • Kiwango cha wadudu wanaosababisha magonjwa wanaokuwepo
  • Ugonjwa unaweza kuenea kwa kiwango gani
  • Muda ugonjwa unaoweza kujitengeneza na kuenea.

Kwa kawaida kukua na kuwepo kwa mlipuko hutegemea njia zinazofahamika. Katika hatua za mwanzo ueneaji huwa ni wa taratibu. Wakati huo kunakuwepo na kinga, hivyo maambukizi yanakuwa ni kidogo. Maambukizi yanapokuwa yameshika kasi, madhara mengine kama vile kutu hutokea mara moja na kuongezeka kwa haraka.

Baadaye, maambukizi hupungua inapokuwa hakuna tena mmea wa kueneza ugonjwa, (hapa mimea yote huwa na ugonjwa), au kama mazingira hayatatoa ushirikiano kwa ugonjwa husika kuendelea kuenea, au kama msimu wa zao husika utafikia mwisho.

Mbinu za kudhibiti magonjwa

  • Mzunguko wa mazao ni moja wapo ya njia nzuri sana za udhibiti wa magonjwa, hii ni kwa sababu aina flani ya wadudu hushambulia na kuathiri aina moja tu ya mazao.
  • Usafi wa mazingira hutegemeana na shughuli za kitaalamu za kilimo zinazolenga kutokomeza au kupunguza vichocheo vya maambukizi kwenye mimea au kwenye shamba. Hii inajumuisha kuondoa na kuharibu mabaki yote ya mavuno ambayo wadudu wanaweza kuishi pamoja na magugu yanayoweza kuwa wenyeji wa wadudu hao.
  • Magonjwa pia yanaweza kupunguzwa au kudhibitiwa kwa kupanda aina ya mazao yenye uwezo wa kukabiliana na magonjwa au yanayovumilia magonjwa.
  • Unaweza kubadilisha muda wa kupanda aina fulani ya mazao, ili kukwepa kipindi ambacho huwa na kiwango kikubwa cha mlipuko wa aina fulani ya magonjwa.
  • Wakati huo huo aina fulani ya mimea huwavutia aina tofauti ya wadudu na magonjwa ambayo baada ya muda fulani hujijenga katika eneo hilo.
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *