Zipo aina nyingi za takataka zin-azoweza kutumika kwa ajili ya kuzalisha mbolea ya mboji kama vile mabaki ya malisho, unga wa maranda unaotokana na shughuli za useremala, majivu na masalia ya ziada baada ya kuvuna mazao shambani.
Kwa kutengeneza mboji, kiasi cha mbolea kitakachopelekwa shambani kitaongezeka kwani samadi itachanganywa na takataka zingine na kuozeshwa.
Ni jambo zuri zaidi kama mkulima utaamua kuhifadhi mbolea ya mboji kwa muda kabla ya kuitumia shambani.
Njia rahisi za kutengeneza mbolea ya mboji
Kuchimba mitaro myembamba shambani Hii ni njia rahisi ambayo mkulima atatakiwa kuchimba ama kutengeneza mitaro myembamba shambani na kisha kuweka kiasi kidogo cha samadi hii ikiwa ni pamoja na ile inayomiminika kutoka kwenye mtambo wa baiyogesi, kisha kufunika samdi hiyo kwa kutumia masalia ya mazao shambani, magugu yaliyofyekwa au kung’olewa, majivu, unga wa mbao pamoja na takataka zingine zinazoweza kuoza taratibu kwenye mitaro hiyo.
Baada ya kufanya hivyo, otesha mazao ya muda mfupi pembeni yam taro na baada ya muda utagundua kuwa mazao yako yanastawi vizuri.
Iwapo utaamua kumwagilia mimea iliyooteshwa kwa utaratibu huu, basi weka maji katika mitaro hiyo. Wakati wa kulima baada ya kuvunamazao, changanya taka zilizoko kwenye mtaro na udongo na kisha chimba mitaro kwa upya na baadaye weka taka ambazo bado hazijaoza kwenye mitaro hiyo na tena rudia zoezi zima toka mwanzo.
Faida ya kutumia njia hii
Itarahisisha uwezekano wa mimea kutumia virutubisho kila vinapopatikana kutoka kwenye taka zinazooza.
Njia hii inaepusha ulazima wa kutengeneza mboji kwa kulundika samadi mahali pazuri na kufunika kwa ajili ya matumizi pale itakapohitajika.
Kuchimba shimo maalumu
- Ili kuongeza kasi ya kufanyika kwa mbolea ya mboji, chimba shimo ardhini lenye urefu wa mita 2, upana wa mita 1 na kina cha mita 1.
- Katika shimo hilo tanguliza masalia yanayotokana na mavuno kutengeneza tabaka la kwanza, kisha weka taka za aina nyingine ili kufanya tabaka la pili na kisha ongeza aina nyingine za taka kufanya tabaka la tatu.
- Endelea kufanya hivyo kwa kuongeza kufuatanisha matabaka mpaka shimo litakapojaa na baada ya kujaa, funika kwa udongo kidogo wenye kina kifupi.
- Kila baada ya sikutatu,nyunyizia lita 50 za maji na geuza taka hizo baada ya majuma mawili ili kufanya za juu kwenda chini na za chini kuja juu ili kuchanganyika vizuri.
- Baada ya majuma mannechanganganya kwa kuzigeuza tena taka hizo nakuzifunika kisha kuchomeka fito moja katikati ya shimo hilo kwa ajili ya kupima kama mbolea yako tayari.
- Baada ya majuma sita chomoa fito hiyo na utakapoikuta haina joto basi mboji yako tayari imeiva na unaweza kuipeleka shambani kwa matumizi.
Kulundika samadi mahali pamoja
Hii ni njia nyingine ya tatu ambayo mkulima anaweza kutumia kutengeneza mboji kwa kulundika samadi mahali pazuri na kisha kufunika na kuacha kuiva na kutumia baadaye.
Samadi inayolundikwa kwa nia hii huweza kutoa virutubiso kwa wingi zaidi kwa ajili ya mimea kuliko ile ambayo haikulundikwa kwa muda maalumu.
Eneo la kulundika samadi hii isiwe karibu na banda la mifugo kwani inzi huweza kuzaliana na kuleta usumbufu kwa kung’ata mifugo yako.