Udongo wenye afya ni udongo ulio hai, ambao unazalisha mazao bora na yenye afya.
Udongo lazima uwe na minyoo na viumbe vingine. Viumbe hawa hufanya kazi ya kulainisha udongo kwa kuvunjavunja masalia ya majani, mimea na mabua yaliyokufa kisha kubeba masalia hayo hadi chini ya udongo na kuichanganya kisha kuzalisha virutubishi vya kwenye mimea.
Viumbe hawa huongeza kasi ya kuoza kwa masalia hayo, na kutoa virutubisho vya mimea. Licha ya hivyo viumbe hai hushindana na viumbe hatari vinavyoweza kusababisha magonjwa kwenye mazao.
Hakuna mavuno bora kwenye udongo wenye afya duni au usiokuwa na rutuba hivyo mkulima kabla hujawaza mavuno fikiria kwanza afya ya udongo kwenye shamba lako.
Ni vyema kufanya kilimo hifadhi kwani hufanya udongo uwe na afya na hutoa mavuno mengi. Hii ni kwasababu hufanya muundo bora wa udongo hivyo kuruhusu mizizi kuingia kwenda chini zaidi na maji kuzama kwenye udongo. Pia huongeza viumbe hai zaidi watakaochakata mabaki mimea na kufanya virutubisho vya mimea kupatikana kwa wingi.