- Kilimo, Kilimo Biashara, Udongo

Rutuba ya udongo ndiyo msingi wa kilimo hai

Sambaza chapisho hili

Kwa muda mrefu sasa tumekuwa mstari wa mbele katika kuzungumzia na kuhimiza uzalishaji kwa misingi ya kilimo hai, ikiwa ni moja ya nguzo za kilimo endelevu.

Katika makala zote zilizochapishwa katika jarida hili pamoja na machapisho mengine yanayotolewa na Mkulima Mbunifu, tumehimiza pia matumizi sahihi ya dawa za asili na mbolea za asili.

Hii inatokana na ukweli kwamba, huwezi kusema unafanya kilimo hai, lakini urutubishaji wa udongo kwa hauzalisha na kutumia mbolea za asili kama vile mboji, samadi, mbolea vunde na nyinginezo.

Si lazima kuwa uzalishe zote kwa pamoja lakini ni muhimu sana kuzalisha mojawapo au mbili ya mbolea hizi na kuwa nayo shambani mwako ikiwa kama nguzo ya rutuba katika shamba lako.

Aidha, tumeona umuhimu wa kukumbushia juu ya urutubishaji wa udongo kwa kuzalisha mbolea za Wanyama na mimea.

Katika kufanikisha hilo, ni muhimu kuhakikisha kuwa unapata taarifa sahihi na unafuata misingi inayoelekezwa, ili kuwa na ufanisi katika uzalishaji.

Huwezi kufanya kilimo hai bila kuwa na uelewa sahihi, au kutokupata maelekezo yanayofaa namna ambavyo unaweza kuzalisha kwa ufanisi.

Tunasisitiza kuwa ni vizuri ukatenga muda na kusoma kwa umakini makala zilizopo katika jarida hili ikiwepo makala ya palizi ya mahindi kwani ndiyo msimu wenyewe umewadia ili uwe na uelewa mpana na hatimae uweze kufanikiwa kama ambavyo umekusudia.

Kumbuka, hakuna kilimo hai bila urutubishaji sahihi wa udongo kwa kutumia mbolea za asili au malighafi za asili zinazopatikana katika maeneo yako.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *